Arejea shuleni baada ya rafiki yake kuwa makamu wa rais

Abdullahi Yusuf Kariye, 56, amerejea shuleni
Abdullahi Yusuf Kariye, 56, amerejea shuleni
Image: BBC

Abdullahi Yusuf Kariye, baba mwenye umri wa miaka 56 mkazi wa eneo la Jigjiga nchini Somalia, ameamua kurejea shuleni miaka thelathini baada ya kukatiza masomo.

Amekuwa akiwalea na kuwasomesha Watoto wake 11. Wanne kati ya watoto wake wana shahada ya chuo kikuu.

Wakati mmoja Abdullahi alikuwa na ndoto ya kurejea shuleni. Mwaka 1987 alimaliza masomo ya shule ya sekondari katikamji wa Hargeisa.

Mkuu wa shule alikuwa Rafiki yake mkubwa wa utotoni.

Katika mwaka 2018 alirejea tena shuleni akajiunga na shule ya sekondari ya Sheikh Abdisalam iliyopo Jigjiga, ambako alipokelewa na mkuu wa shuleAbdulkadir Abdirahman Ahmed, aliyesoma na Abdullahi Yusuf Kariye.

Mwaka 2021 alimaliza masomo yake na akawezakupata stashahada ambayo ilimuwezesha kusoma Chuo kikuu.

Abdullahi alijiunga na Chuo kikuu cha Jigjigakusomea masomo ya uhandisi wiki hii.