Rais wa Malawi amvua naibu mamlaka juu ya ufisadi

Muhtasari

• Hii ni kuhusiana na kandarasi 16 ambazo Huduma ya Polisi ya Malawi na Jeshi la Ulinzi la Malawi zilitoa kwa kampuni tano za Bw Sattar.

• Makamu wa rais bado hajajibu tuhuma hizo.

• Bw Chakwera aliungana na Bw Chilima kumshinda Peter Mutharika katika uchaguzi wa urais wa 2020.

Image: AFP

Rais wa Malawi Lazarus Chakwera amemvua makamu wake Saulos Chilima mamlaka yote aliyokabidhiwa baada ya kutajwa katika kashfa ya ufisadi ya $150m (£123m) iliyohusisha kandarasi za serikali.

Makamu wa rais bado hajajibu tuhuma hizo.

Ripoti ya Taasisi ya Kupambana na Rushwa nchini (ACB) iliwataja maafisa 53 wa sasa na wa zamani kuwa walipokea pesa kutoka kwa mfanyabiashara kutoka Uingereza na Malawi Zuneth Sattar kati ya 2017 na 2021, rais alisema.

Hii ni kuhusiana na kandarasi 16 ambazo Huduma ya Polisi ya Malawi na Jeshi la Ulinzi la Malawi zilitoa kwa kampuni tano za Bw Sattar.

Maafisa waliotajwa kwenye ripoti hiyo ni pamoja na makamu wa rais na mkuu wa polisi - ambaye amefutwa kazi.

Lakini sheria ya Malawi hairuhusu rais kumfukuza kazi au kumsimamisha kazi makamu wake kwa vile rais huyo ni afisa aliyechaguliwa.

"Kila bora ninachoweza kufanya kwa sasa, ambacho nimeamua kufanya, ni kunyima afisi yake majukumu yoyote aliyokabidhiwa huku nikisubiri ofisi ithibitishe madai dhidi yake," rais alisema katika hotuba ya kitaifa Jumanne.

Bw Chakwera aliungana na Bw Chilima kumshinda Peter Mutharika katika uchaguzi wa urais wa 2020. Wawili hao walikuwa wameahidi kupambana na ufisadi serikalini.