logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Tetemeko la ardhi Afghanistan: Takriban watu 250 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika mkoa wa Paktika

Tetemeko kubwa la ardhi limesababisha vifo vya takriban watu 250 na wengine wengi kujeruhiwa.

image
na Radio Jambo

Burudani22 June 2022 - 06:27

Muhtasari


• Tetemeko hilo lilipiga takriban kilomita 44 kutoka mji wa kusini-mashariki wa Khost.

• Mitetemeko ilisikika katika zaidi ya kilomita 500 za Afghanistan, Pakistan na India, kulingana na Kituo cha Ulaya cha Seismological Center, kilichonukuliwa na Reuters.

Tetemeko kubwa la ardhi limesababisha vifo vya takriban watu 250 na wengine wengi kujeruhiwa nchini Afghanistan, afisa mmoja wa eneo hilo ameiambia BBC.

Picha zilizoshirikiwa kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha watu wakiwa kwenye machela, vifusi na nyumba zilizoharibika katika jimbo la Paktika.

Afisa wa serikali ya eneo hilo aliambia BBC kwamba idadi ya waliofariki zaidi ya 250 huenda ikaongezeka, na kwamba wengine zaidi ya 150 wamejeruhiwa.

Tetemeko hilo lilipiga takriban kilomita 44 kutoka mji wa kusini-mashariki wa Khost.

Mitetemeko ilisikika katika zaidi ya kilomita 500 za Afghanistan, Pakistan na India, kulingana na Kituo cha Ulaya cha Seismological Center, kilichonukuliwa na Reuters.

Kituo hicho kilisema kuwa mashahidi wameripoti kuhisi tetemeko hilo katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul, pamoja na mji mkuu wa Pakistan, Islamabad.

"Kwa bahati mbaya, jana usiku kulitokea tetemeko kubwa la ardhi katika wilaya nne za mkoa wa Paktika, ambalo liliua na kujeruhi mamia ya wananchi wetu na kuharibu makumi ya nyumba," msemaji wa serikali Bilal Karimi alitweet.

"Tunaomba mashirika yote ya misaada kutuma timu katika eneo hilo mara moja ili kuzuia maafa zaidi."

Tetemeko hilo - ambalo lilipiga saa za mapema wakati watu wengi walilala - lilikuwa tetemeko la kipimo cha 6.1 katika kina cha kilomita 51, kulingana na Utafiti wa Jiolojia wa Marekani.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved