logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Severodonetsk:Vikosi vya Ukraine vyaagizwa kuondoka kutoka mji muhimu wa mashariki

Miundombinu yote ya jiji imeharibiwa, na zaidi ya 90% ya nyumba zimepigwa makombora

image
na Radio Jambo

Habari24 June 2022 - 11:40

Muhtasari


• Vikosi vya Ukraine vilivyoko Severodonetsk vimetakiwa kuondoka, kwa mujibu wa afisa wa ngazi ya juu wa eneo hilo.

Vikosi vya Ukraine vilivyoko Severodonetsk vimetakiwa kuondoka, kwa mujibu wa afisa wa ngazi ya juu wa eneo hilo.

Mji huo ndio kitovu cha uvamizi wa Urusi huku Moscow ikijaribu kuchukua udhibiti wa sehemu kubwa za mashariki mwa Ukraine.

"Kusalia katika nafasi ambazo zimeshambuliwa kwa miezi mingi haina maana," gavana wa mkoa wa Luhansk Serhiy Haidai alisema.

Vikosi vya Urusi vimepiga hatua katika siku za hivi karibuni na vinakaribia kuzunguka jiji hilo, na mji wake pacha wa Lysychansk.

"Wamepokea maagizo ya kurejea kwenye nafasi mpya... na kutoka huko waendelee na shughuli zao," Bw Haidai aliambia televisheni ya Ukraine.

"Hakuna maana ya kukaa katika nafasi ambazo zimeharibiwa kwa miezi kadhaa kwa sababu ya kubaki," alisema.

Miundombinu yote ya jiji imeharibiwa kabisa, Bw Haidai aliongeza, na zaidi ya 90% ya nyumba zikiwa zimepigwa makombora na 80% kuharibiwa vibaya.

Uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine, ulioanza mnamo Februari, umekuwa ukilenga Severodonetsk na mji wake pacha wa Lysychansk kwa wiki kadhaa.

Ni nafasi za mwisho zilizosalia za Kiukreni katika eneo la Luhansk, moja ya mikoa miwili inayounda Donbas ya mashariki.

Rais wa Urusi Vladimir Putin amedai kwa uwongo kwamba wazungumzaji wa Kirusi katika Donbas wamekuwa wahanga wa mauaji ya halaiki - mojawapo ya sababu kuu anazotumia kuivamia Ukraine.

Siku ya Alhamisi, vikosi vya Urusi vilichukua udhibiti wa maeneo zaidi kusini mwa Severodonetsk na Lysychansk, na kuzua hofu kwamba vikosi vya Ukraine vitazingirwa huko hivi karibuni.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved