Sri Lanka: Waziri Mkuu ateuliwa kuwa rais wa mpito

Hatahivyo, hakuna neno la moja kwa moja kutoka kwa rais Rajapaksa mwenyewe

Muhtasari

• Matangazo yote katika siku za hivi karibuni yametoka kwa spika wa bunge na ofisi ya waziri mkuu.

Image: BBC

Waziri Mkuu wa Sri Lanka Ranil Wickremesinghe ameteuliwa kuwa Rais wa muda, kulingana na spika wa bunge.

Waziri Mkuu ameteuliwa kuwa Kaimu Rais: Spika alisema Rais Gotabaya Rajapaksa alimfahamisha kuhusu uteuzi huo chini ya Kifungu cha 37.1 cha katiba ya Sri Lanka.

Hatahivyo, hakuna neno la moja kwa moja kutoka kwa Rajapaksa mwenyewe.

Matangazo yote katika siku za hivi karibuni yametoka kwa spika wa bunge na ofisi ya waziri mkuu.

Kwa mujibu wa Katiba ya Sri Lanka, nafasi ya rais ikiwa wazi, waziri mkuu ataapishwa na kukaimu kwa muda mpaka atakapochaguliwa rais kutoka miongoni mwa wabunge.

Uchaguzi huo unapaswa kufanyika ndani ya siku 30 baada ya Rais kujiuzulu. Spika wa bunge la Sri Lanka alisema uchaguzi unaweza kufanyika Julai 20, 2022.

Rais wa Sri Lanka Gotabaya Rajapaksa ameikimbia nchi hiyo kwa ndege ya kijeshi, huku kukiwa na maandamano makubwa kuhusu mzozo wa kiuchumi.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 73 amekimbilia Maldives.