Ivana Trump, mke wa zamani wa Rais wa zamani Donald Trump, ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 73, kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa watoto wake Donald Trump Jr., Ivanka Trump na Eric Trump.
''Ni kwa masikitiko makubwa kutangaza kifo cha mama yetu mpendwa," Ivan Trump alisema kwa taarifa, "Mama yetu alikuwa mwanamke aliyemiliki biashara na kando na hayo,pia alikuwa mwanariadha wa kiwango cha kimataifa, mama alikuwa na mapenzi ya dhati kwa watu na kujali na rafiki zake,"
Mwanariadha huyo amewacha pengo kubwa kwa familia yake ya watoto wa tatu na wajukuu kumi.
Donald, ambaye alikuwa bwana wa Ivana kutoka 1977 hadi 1992, pia hakuficha hisia zake kumwomboleza bibi yake huyo wa zamani.
"Nina huzuni kubwa kuwajulisha wote waliompenda, ambao ni wengi, kwamba Ivana Trump amefariki nyumbani kwake huko New York City," aliandika. "Alikuwa mwanamke mzuri, mrembo, na wa kushangaza, ambaye aliishi maisha mazuri,"
Aliongeza kwa kusema kuwa , "Fahari na furaha yake ilikuwa watoto wake watatu, Donald Jr., Ivanka, na Eric. Aliwajivunia sana,Mungu alaze roho wake pahali pema peponi,"
Kulingana na Afisa wa jiji la New York walisema kuwa Ivana alipatikana amekufa ndani ya nyumba yake Manhattan mnamo Julai 14.
Mwili wa mwendazake ilipelekwa kwa hospitalini kwa Mkuguzi wa Afya ili kubaini chanzo cha kifo chake.