Kasisi afariki akiongoza ibada ya mazishi

Kasisi huyo alikuwa akiongoza hafla ya mazishi ya mmoja wa wapendwa wao ghafla akadondoka ardhini na kuzimia.

Muhtasari

• Kasisi huyo wa kanisa katoliki alidondoka msibani na kuzimia ghafla.

• Alipokimbizwa hospitalini, alitangazwa kufariki.

Maziara
Maziara
Image: The Star

Kasisi mmoja kutoka nchini Tanzania ametangazwa kufa wakati anaongoza ibada ya wafu katika mazishi ya mmoja wa waumini wa kanisa katoliki jimbo alikokuwa akihudumu.

Kasisi huyo kwa jina Laurence Milanzi wa kanisa Katoliki kijiji cha Liputu, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara, alifariki Dunia maeneo ya makaburini alipokuwa akishiriki mazishi ya mwanakijiji mwenzao aitwae Daudi Veno.

Waliuoshuhudia tukio hilo la kusikitisha na kuchapisha taarifa hizo kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii walisema kasisi Milanzi alianguka ghafla waakti alipokuwa akiwqazungumzia watu umuhimu wa kuhudhuria misiba ya wenzao pindi wanapotangulia mbele za haki.

Kifo hicho kilichotokea kwenye msiba kilikuwa tukio moja baya zaidi linalotafiriwa kama matukio kwenye filamu ambapo Jumanne mchana was aa tano asubuhi kasisi alimfuata mpendwa wao ambaye alikuwa akimuaga buriani.

Mwili wake ulihifadhiwa katika Hosptali ya Mission ya Ndanda, Wilaya ya Masasi ukisubiri taratibu za mazishi yanayotarajiwa kufanyika Kijiji hapo, baada ya kukamilika kwa taratibu zote.

Baadhi ya mashuhuda walioudhuria mazishi ya Daudi Veno, wameeleza kwamba, kasisi Milanzi alikutwa na umauti huo, alipokuwa anatoa sala na kuwasihi viongozi wenzake wa Dini kuacha tabia ya kutohudhuria mazishi kwa Binadamu mwenzao asiyeshiriki masuala ya Ibada.

Mchungaji Milanzi alisema kitendo cha kususa kumuombea marehemu kwa kuwa hakuwa anashiriki kwenye Nyumba za Ibada, Kanisani na misikitini ni kwenda kinyume na maagizo ya mwenyezi Mungu alivyoagiza mtu anapofariki ni muhimu akazikwa na sio kumuacha kwani uharibu hali ya hewa kutokana na harufu mbaya kutoka kwake.

“Baada ya kueleza hayo, tukamuona mwenzetu akidondoka chini kisha kupoteza fahamu” waliokuwepo walieleza.

Aidha,mashuhuda hao wamesema kwamba baada ya Mchungaji huyo kudondoka chini walimchukuwa na kumkimbiza Hosptali ya Ndanda na kuelezwa na madaktari kuwa alishafariki