Wanajeshi 15,000 wa Urusi wameuawa vitani Ukraine: Mkurugenzi wa CIA

CIA imesema makadirio ya hivi karibuni ni kwamba Urusi imewapoteza watu 15,000 na mara tatu ya idadi hiyo walijeruhiwa .

Muhtasari

• Mkurugenzi wa CIA William Burns alisema kuna uvumi mwingi kuhusu hali ya afya ya Putin, lakini wanavyojua , afya yake ni nzuri.

Mkurugenzi wa CIA William Burns
Mkurugenzi wa CIA William Burns
Image: BBC

Mkurugenzi washirika la ujasusi la Marekani (CIA )William Burns amesema kuwa: "Makadirio ya hivi karibuni kutoka ujasusi wa marekani ni kwamba Urusi imewapoteza watu 15,000 katika vita vya Ukraine na mara tatu ya idadi hiyo walijeruhiwa ."

Taarifa hiyo imechapishwa katika jukwaa la usalamala Aspen , na vyombo vya habari vya Reuters na CBS.

"Na Ukraine pia labda iliumiwa -kidogo, lakini bado , unafahamu, vifo hivi ni muhimu," aliongeza Mkurugenzi wa CIA.

Kulingana na ujumbe wa Twitter, mwandishi wa wa CBS, Mkurugenzi wa CIA alipoulizwa kuhusu hali ya Putin alisema: "Kuna uvumi mwingi kuhsu hali ya afya ya Putin, lakini tunavyojua , afya yake ni nzuri zaidi ," Alisema Burns.

Kwingineko;

Makombora ya ‘’Uturuki’’ yalipigwa na Iraqi na kusababisha vifo na majeruhi

Image: BBC

Raia tisa , wakiwemo watoto wawili, wameuawa na wengine 33 kujeruhiwa katika shambulio la kombora la Uturuki katika jimbo la Dohuk kaskazini mwa Iraq, kwa mujibu wa maafisa.

Televisheni ya Iraqi iliripoti kuwa "shambulio zito" lilipiga hoteli ya kifahari katika mji wa Zakho, ambao uko kwenye mpaka wa Kurdistan baina ya nchi hiyo na Uturuki.

Shirika la habari la Iraq limesema kuwa watu wote waliokufa walikuwa ni watalii.

Maafisa wa Iraqi wameishutumu Uturuki kwa shambulio hilo, lakini serikali mjini Ankara imekana kuhusika na tukio hilo.

Mkuu wa jimbo la Zakho , Mushir Bashir, alisema kuwa wengi wa waliokufa walikuwa ni "watalii wa kiarabu kutoka Iraqi, wengi wao kutoka maeneo ya kati na kusini mwa nchi ".

"uturuki ilikipiga kijiji mabomu mara mbili kwa siku",alinukuliwa akiliambia shirika la habari la AFP.