Bendera yazua utata baada ya wanariadha wa Ethiopia kushinda mbio za mita mita 5,000

Shabiki alikimbilia uwanjani akiwa amebeba kile kilichoonekana kuwa bendera ya Tigray.

Guday Tsegay alishinda medali ya dhahabu katika mbio za mita 5,000 katika mashindano ya dunia ya riadha nchini Marekani Jumapili.
Guday Tsegay alishinda medali ya dhahabu katika mbio za mita 5,000 katika mashindano ya dunia ya riadha nchini Marekani Jumapili.
Image: BBC

Muethiopia Guday Tsegay alishinda medali ya dhahabu katika mbio za mita 5,000 kwa wanawake siku ya Jumapili lakini ushindi wake ulikumbwa na utata baada ya shabiki kukimbilia uwanjani akiwa amebeba kile kilichoonekana kuwa bendera ya Tigray.

Shabiki huyo aliwanyanyua wanariadha wote wa Ethiopia, Guday Tsegay na Dawit Seyaum - ambao walimaliza wa tatu - kabla ya kuondolewa uwanjani kwa ajili ya usalama.

Serikali ya Ethiopia ilianzisha oparesheni ya kijeshi mwezi Novemba 2020 katika eneo la Tigray kaskazini mwa nchi.

Hatua hiyo Ilifuatia mzozo kati ya serikali ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed na TPLF, chama kikuu cha kisiasa cha Tigray.

Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilizuka, na baadaye kusababisha mzozo mkubwa wa kibinadamu.