logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Askofu aibiwa vito vya thamani ya dola milioni moja wakati wa mahubiri

Miongoni mwa vitu alivyoibiwa ni pamoja na saa aina ya Rolexes, almasi na zumaridi.

image
na Radio Jambo

Burudani27 July 2022 - 04:48

Muhtasari


•Miongoni mwa vitu alivyoibiwa, mhubiri huyo anayeendesha gari aine ya Rolls Royce ni saa aina ya Rolexes, almasi na zumaridi.

Mhubiri anayejulikana kwa mtindo wake wa maisha ya ufahari ameibiwa vito vya thamani ya zaidi ya $1m (£840,000) wakati wa mahubiri yaliyopeperushwa moja kwa moja katika jiji la New York.

Lamor Whitehead, 44, ameapa kwamba wahalifu "hawataepuka"

Miongoni mwa vitu alivyoibiwa, mhubiri huyo anayeendesha gari aine ya Rolls Royce ni saa aina ya Rolexes, almasi na zumaridi.

Polisi bado wanachunguza tukio hilo. Mpaka sasa hakuna mshukiwa ambaye ametajwa wala kukamatwa.

Katika video hiyo Bw Whitehead anasikika akiuliza "Ni wangapi kati yenu mmepoteza imani kwa sababu mliona mtu mwingine akifa?" muda mfupi kabla ya watu kadhaa waliovalia nguo nyeusi kuingia kanisani huko Brooklyn.

"Nilipowaona wakiingia kwenye hekalu na bunduki zao, nilimwambia kila mtu [alale] chini, kila mtu alale," baadaye alisema kwenye ukurasa wa Instagram."Sikujua kama walitaka kulipiga risasi kanisa au kama walikuwa wanakuja kwa wizi."Kulingana na Bw Whitehead, wezi hao waliojifunika nyuso zao walitoroka kwa kutumia gari aina ya Mercedes.

Kufuatia wizi huo, gazeti la New York Post liliripoti kuwa vitu vilivyochukuliwa kutoka kwake na mkewe ni pamoja na saa za Rolex na Cavalier za $75,000, rubi ​​ya Episcopal ya $25,000 na pete ya almasi na pete za $25,000 - na hata pete yake ya harusi.

BBC imewasiliana na Bw Whitehead ili kupata maoni yake.

Katika taarifa, meya wa jiji la New York Eric Adams - ambaye amemfahamu Bw Whitehead tangu mwaka 2013 - alisema kuwa Idara ya Polisi ya New York ilikuwa ikichunguza uhalifu huo.

"Hakuna mtu katika jiji hili anayepaswa kuwa muathiriwawa wizi wa kutumia silaha, achilia mbali viongozi wetu wa kidini," Bw Adams alisema.

Bw Whitehead, kwa upande wake, ametoa zawadi ya dola 50,000 kwa atakayetoa habari zitakazowezesha kukamatwa.

Tukio la hivi punde, hata hivyo, lilizua ukosoaji mwingi kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kupenda anasa na maisha ya kifahari.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved