"Nisamehe kwa yaliyotokea!" Mwalimu amuua mkewe na kuachia wakwe zake ujumbe kabla ya kujiua

Mwalimu huyo alimuhadaa mkewe kwenda chumba cha wageni katika hoteli moja ambapo alimuua.

Muhtasari

• Baada ya kumuua mkewe kwenye gesti, inasemekana mwalimu huyo naye alijiua baadae katika eneo tofauti kabla ya kuwaachia ndugu za mke wake ujumbe wa kutaka kusamehewa.

Kamba ya kujiua
Kamba ya kujiua
Image: Image: Courtesy

Visa vya maujai haswa katika mahusiano na ndoa vinazidi kukithiri huku baadhi ya wataalamu wakidai kwamba ni msongo wa mawazo na wengi wa wapenzi kuathirikika afya ya akili.

Nchini Tanzania, kisa cha kuliza mno kiliwasabahi wakaazi wa la Tanga baada ya kupata taarifa kwamab mwalimu mmoja aliyetambulika kwa jina Emmanuel Jerome alichukua hatua ya kumuua kwa kumnyonga mkewe katika chumba cha hoteli na kisha baadae kujiua pia kwa kujinyonga katika eneo tofauti kwa jina Katavi.

Kamanda wa polisi katika eneo la Katavi alidhibitisha matukio haya ya kusikitisha na kusema kwamba inaonekana ni wivu tu wa kimapenzi uliosababisha mwalimu huyo kumuua mpenzi wake baada ya kumhandaa Kwenda chumba cha hoteli almaarufu gesti na kumtendea unyama huo kabla yake mwenyewe pia kujisafirisha jongomeo kwa kutumia Kamba.

Alisema Jerome na mkewe walipanga safari kuelekea mkoani Rukwa, ambapo ni nyumbani kwao marehemu mke wake na walifikia nyumba ya kulala wageni Julai 26, 2022, ndipo usiku alipochukua uamuzi wa kumnyonga mkewe

Kamanda huyo wa polisi alisema baada ya kumnyonga katika nyumba hiyo ya wageni, aliacha ujumbe wa maandishi kwa ndugu wa mke wake uliosomeka: "Nisameheni kwa yaliyotokea".

Alieleza kuwa baada ya kufanya tukio hilo mkoani Rukwa alikimbilia mkoani Katavi na Julai 27,2022 usiku, alichukua uamuzi wa kujinyonga na walikuta mwili wake ukiwa unaning'inia kwenye kamba.

Wananchi mbali mbali waliokasirishwa na kitendo hicho walitoa kauli za kughadhabisha mno huku wakilaumu watu wanaoingia katika ndoa hali ya kuwa hawajamaliza starehe za ujanani kupelekea kuanza kuchepuka na matokeo yake ni kuuana kinyama.

“Wanaume tunakwama wapi? Kama ameamua kudanga si unampatia talaka awe huru kabsa warembo wamejaa tele tena wenye hofu ya mungu unajiua mtumishi mzima maamuzi ya hovyo kabisa,” mmoja kwa jina Anderson Mafie alisema.