Baharia akaa saa 16 baharini baada ya boti yake kupinduka Atlantiki

Hali ya bahari ilikuwa mbaya sana kwa baharia huyo kuokolewa kwa hivyo alilazimika kungoja hadi asubuhi.

Muhtasari

•Mwanaume mwenye umri wa miaka 62 amekaa kwa saa 16 baharini kwa kutumia puto lenye hewa ndani ya boti yake baada ya kupinduka

Image: BBC

Mwanamume mmoja wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 62 amekaa kwa saa 16 baharini kwa kutumia puto lenye hewa ndani ya boti yake baada ya kupinduka.

Chombo chake chenye urefu wa mita 12, kilikuwa kimeanza safari kutoka mji mkuu wa Ureno Lisbon, kilituma ishara ya kupata shida Jumatatu jioni kutoka Bahari ya Atlantiki.

Walinzi wa pwani wa Uhispania waliiona mashua iliyopinduka lakini hali ya bahari ilikuwa mbaya sana kwenda kuokoa kwa hivyo baharia alilazimika kungoja hadi asubuhi.

Kunusurika kwa mwanamume huyo "kunaelekea kuwa jambo lisilowezekana", walisema walinzi wa pwani.

Boti yake ilituma ishara ya kupata tatizo saa mbili usiku siku ya Jumatatu, maili 14 (kilomita 22.5) kutoka Visiwa vya Sisargas, karibu na eneo la kaskazini-magharibi la Galicia nchini Uhispania.

Meli ya uokoaji iliyokuwa imebeba wapiga mbizi watano pamoja na helikopta tatu ilienda kumtafuta na kumuokoa mtu huyo ambaye bado hajatajwa jina.

Mpiga mbizi muokoaji alibana kwenye sehemu ya meli ili kuangalia kama kuna dalili za mtu kuwa hai na mtu huyo akajibu kwa kugonga chombokutoka ndani.

Bahari ilikuwa imechafuka na jua lilikuwa limetua kwa hiyo timu ya waokoaji iliambatanisha puto zinazopepea hewani kwenye mashua ili isizame na kungoja hadi asubuhi.

Siku iliyofuata, wapiga mbizi wawili waliogelea chini ya mashua ili kumsaidia baharia huyo kutoka