Serikali ya Uganda yapiga Marufuku Wasanii kutumbuiza wanafunzi Shuleni

Wizara ya Elimu na Michezo Uganda imepiga marufuku wasanii kuzuru mashule

Muhtasari

•Haya yanajiri baada ya mwezi uliopita Mbunge wa Tororo Sarah Acheing Opendi kuliambia bunge kuwa kiwango cha wanamuziki kueneza uasherati shuleni ni cha kutisha na hivyo akatoa wito wa kupigwa marufuku kwa wanamuziki wa kilimwengu kutumbuiza shuleni.

Mwanamuziki kwa jukua
Mwanamuziki kwa jukua
Image: Handout

Wizara ya Elimu na Michezo Uganda  imepiga marufuku mara moja kwa shughuli zozote zinazohusiana na  wanamuziki kutumbuiza wanafunzi  katika Shule za Msingi na Sekondari.

Marufuku hiyo ambayo inaanza kutumika mara moja itatekelezwa katika shule za msingi na sekondari za serikali na za kibinafsi.

Haya yamo katika waraka ambao ulitolewa kwa walimu wakuu na Wakuu wote wa shule na Dk Jane Okou kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara.

"Walimu wakuu na Wakuu wa Shule zote za Msingi na Sekondari wanaonywa kutoajiri au kuruhusu yeyote kati ya "wasanii" hawa kufanya maonyesho shuleni. Wasimamizi wa shule wanapaswa kuwajibika na kudii maagizo haya, yule ambaye atapatikana kuenda kinyume na hii maagizo atachukuliwa hatua''  Agizo kutoka katika waraka hiyo.

Wizara pia ilibainisha kuwa shughuli za ziada shuleni kwa kawaida kama vile michezo na uimbaji, vilabu vya mijadala, n.k na ikiwa shule zinahitaji kujiliwaza, basi zinaweza kushiriki katika maigizo ya kuigiza au kupanga matamasha.

Haya yanajiri baada ya mwezi uliopita Mbunge wa Tororo Sarah Acheing Opendi kuliambia bunge kuwa kiwango cha wanamuziki kueneza uasherati shuleni ni cha kutisha na hivyo akatoa wito wa kupigwa marufuku kwa wanamuziki wa kilimwengu kutumbuiza shuleni.