(+video) Akamatwa kwa kupiga simu zimamoto kuwatania kisha kuzima

Aliwapigia shirika la zimamoto simu kuwatania kuwa kuna sehemu inateketea kisha akazima simu

Muhtasari

• Alisema kwamba alikuwa anajifurahisha tu kutokana na kuzembea, hakuwa na kazi ya kufanya

Shelida Ibrahim, mwanamke aliyewaita zimamoto na kuzima simu
Shelida Ibrahim, mwanamke aliyewaita zimamoto na kuzima simu
Image: YouTube screengrab

Mara nyinig kuzembea bila kazi kunaweza kukamletea mtu majaribio mengine ya kukufuru kabisa, ndio unaambiwa akili iliyozembea ni himaya ya ibilisi!

Nchini Tanzania katika mkoa wa Geita mwanamke mmoja alitiwa mbaroni baada ya kuwapigia simu shirika la kutoa msaada wa zima moto na kuwapa maelekezi akiwatania kwamba kuna sehemu kunaungua.

Baada ya hapo alizima simu yake na katika kukamatwa kwake alisema kwamba alikuwa anawatania tu kwa kujifurahisha mwenyewe.

Katika taarifa ya habari iliyopeperushwa na kituo kimoja cha rininga nchini humo, mrembo huyo alijitambulisha kwa jina Shelida Ibrahimu mwenye umri wa miaka 20 alikamatwa kwa kosa la kuwapigia simu zimamoto na kuwaambia kuna tukio la moto na baadaye akazima simu yake kwa lengo la kujifurahisha.

Polisi walimtia mbaroni kwa kile walisema kwamba aliwasababishia hasara kubwa ya kuwasha magari kwa haraka mno ili kukimbia kuokoa mali iliyosemekana inateketea, kutoka kwa taarifa ya mrembo huyo.

Mwanadada huyo katika video alijieleza kwamba hajui ni nini kilimtokea kumpa majaribu hayo ya kuwapigia simu shirika la zima moto na ilikuwa mara yake ya kwanza kufanya kitendo hicho.

Aliomba radhi na kutaka kusamehewa kwani kwa maelezo yake hata yeye hajui nini kilimuingia mpaka kuchukua uamuzi huo wa kushtua.

Nilipiga simu kwa Jeshi la Zimamoto niliwatumia taarifa za uongo baada ya hapo walivyotaka maelekezo ili waje mahali nilipo nikazima simu, asubuhi wakanikamata,”

Nilijisikia tu kushika simu na kupiga, sijawahi kupigia zima moto simu mimi. Naomba msamaha kwa jeshi la polisi na zima moto sirudii tena kutumia simu yangu vibaya,” alijieleza kwa majonzi.

Afisa wa Jeshi hilo Inspekta Edward Lukuba amesema Shelida baada ya kutoa taarifa hiyo alisababisha Jeshi hilo liingie hasara ya kuwasha magari na kukimbilia eneo ambalo walidanganywa.

"Leo tumegundua anaitwa Asia au Shelida lakini jana alijitambulisha kama Rehema Mwiti, alipiga simu kwa hisia nyumba inaungua, Askari walitoka baada ya kukaribia yule Dada alizima simu, hakupatikana tena, leo Septemba 6 kupitia Askari wetu tuliweza kumbaini na kumnasa tumefanya nae mahojiano na amekiri hilo kwamba anafanya hivyo kwa kujifurahisha" afisa wa polisi alieleza.