Maelfu ya nyeti za punda wa kiume zimekamatwa zikisafirishwa kwa njia ya kimagendo Kutoka nchini Nigeria Kwenda Hong Kong.
Kulingana na taarifa kutoka taifa hilo lenye wingi wa watu katika bara la Afrika, mamlaka zilitaarifiwa baada ya magunia kadhaa yaliyokuwa yamebeba nyeti hizo zipatazo elfu 7 kukamatwa kweney uwanja wa ndege wa Lagos tayari kusafirishwa Kwenda Uchina mji wa Hong Kong.
Mwenye shehena hiyo anasemekana kwamba alikuwa amedanganya nyeti hizo zilikuwa za ndume ila baada ya ukaguzi wa kina zikagundulika kuwa ni nyeti za punda wa kiume.
Nyeti hizo zilikuwa zimewekwa katika maguni kumi na sita.
Taarifa zinasema kwamba nchini Nigeria kuekuwa na suala la kupatikana kwa Ngozi za punda zikisafirishwa Kwenda mataifa ya mashariki ila hilo la kusafirisha nyeti za punda ni jipya kabisa kuwahi kutokea.
Kulingana na ripoti, harufu kali iliyokuwa ikitoka kwenye mifuko hiyo, ilisababisha maafisa wa forodha kufungua vifurushi na kugundua nyeti 7,000 za punda na zaidi ya vipande 3,000 vya ngozi za punda.
Biashara haramu ya sehemu za punda kwenda China ni ya kawaida sana, hutumiwa katika dawa fulani za Kichina.
Mnamo 2021, maseneta katika taifa hilo walitaka kupitisha mswada wa kuharamisha kuchinjwa kwa punda na kusafirishwa nje kwa bidhaa za Wanyama hao ila taarifa hizo zilisema kwamba mswada huo ungali bado hujapitishwa kuwa sheria.