Mazishi umma ya Malkia Elizabeth II ilivyofanyika

Kipindi cha maombolezo ya kifalme kinaendelea kwa wiki nyingine

Image: BBC

Matukio ambayo yalishuhudiwa jana, Jumatatu huenda yakarudiwa kwa miongo kadhaa ijayo.

Huu hapa muhtasari wa kile kilichotokea:

  • Siku ilianza na hitimisho la kipindi cha uongozi wa Malkia, na msafara wa jeneza lake kuelekea Westminster Abbey.
  • Ibada ya mazishi huko Westminster Abbey ilihudhuriwa na karibu watu 2,000 wakiwemo wakuu wengi wa nchi.
  • Msafara mkubwa kisha ulitembeza jeneza la Elizabeth II hadi Wellington Arch: Alama ya kihistoria yenye umuhimu wa ushindi katika historia ya Uingereza.
  • Malkia aliwekwa kwenye gari maalum la kubeba maiti na kuendeshwa hadi Windsor.
  • Msafara wa tatu wa siku ulimuonyesha tena Mfalme na washiriki wengine wa familia ya kifalme wakitembea nyuma ya gari la maiti la Malkia alipokuwa akipelekwa katika Kanisa la St George kwa ibada ya mwisho iliyohudhuriwa na watu 800.
  • Baadaye  mwendo wa saa 19:30 - Familia ya Kifalme ilirudi kwenye kanisa kwa hafla ya faragha ambapo Malkia Elizabeth alizikwa kando ya marehemu mumewe, Duke wa Edinburgh.
  • Kipindi cha maombolezo ya kifalme kinaendelea kwa wiki nyingine - hadi mwisho wa tarehe 26 Septemba