Urusi na Ukraine: Mtoto asikika akilia 'kwaheri baba' huku babake raia wa Urusi akienda vitani Ukraine

Video hiyo inaonyesha wanaume wa Urusi wanaopanda mabasi kwenda kupigana vitani.

Muhtasari

• Urusi imeanza kutekeleza mipango ya kuwaita askari wa akiba kupigana nchini Ukraine baada ya kukabiliwa vilivyo na wanajeshi wa Ukraine.

Mtoto anasikika akilia huku akimuaga baba yake katika video iliyosambazwa kwenye Telegram. Video hiyo inaonyesha wanaume wa Urusi wanaopanda mabasi kwenda kupigana vitani.

Mwandishi wa BBC Will Vernon aliweza kuthibitisha kanda hiyo baada ya kuzungumza na wenyeji wa Staryi Oskol katika Mkoa wa Belgorod, akiwemo mwanamke mmoja ambaye alikuwepo wakati video hiyo iliporekodiwa. Video hiyo imesambazwa katika programu ya kijamii ya Telegraph.

Urusi imeanza kutekeleza mipango ya kuwaita askari wa akiba kupigana nchini Ukraine baada ya kukabiliwa vilivyo na wanajeshi wa Ukraine.

Rais Vladimir Putin aliamuru kuwasajili Warusi zaidi ya 300,000 wenye uzoefu wa kijeshi, na hivyo kuzua maandamano nchini humo siku ya Jumatano.