Wahudumu 5 wa afya wameambukizwa ebola nchini Uganda

Jumla ya watu ishirini na wanne wamethibitishwa kuambukizwa virusi hivyo nchini, watano kati yao wamefariki.

Muhtasari
  • Jumla ya watu ishirini na wanne wamethibitishwa kuambukizwa virusi hivyo nchini, watano kati yao wamefariki
Image: AFP

Takriban wahudumu wa afya watano wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya Ebola huku mlipuko huo ukiendelea kuenea katika eneo la kati nchini Uganda.

Dkt. Herbert Luswata katibu mkuu wa Chama cha Madaktari Uganda ameambia BBC kwamba wenzake waliambukizwa virusi hivyo katika hatua za kwanza za mlipuko huo wakati ufahamu ulikuwa mdogo na kwamba hawakuwa na vifaa vya kutosha vya kujikinga.

Watano hao kwa sasa wanapokea matibabu katika hospitali ya Mubende, kituo kikuu cha walioambukizwa Ebola.

Jumla ya watu ishirini na wanne wamethibitishwa kuambukizwa virusi hivyo nchini, watano kati yao wamefariki.

Chama cha wafanyikazi wa matibabu hapo awali kilitoa wito kwa maeneo yenye Ebola kuwekwa chini ya karantini ili kukomesha kuenea zaidi kwa ugonjwa wa virusi vya hemorrhagic.

Katika taarifa siku ya Jumanne, wafanyikazi wa matibabu waliofunzwa walisema hawatarejea kazini hadi wote watakapopimwa Ebola na wale waliopatikana wameambukizwa kutoa matibabu.

Wahudumu wa afya walisema wako kwenye mgomo hadi hali zao za kazi zitakapoboreshwa.

Rais Yoweri Museveni anatarajiwa kuhutubia nchi kuhusu mlipuko wa Ebola Jumatano usiku.