logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nitawashinda baada ya baba yangu kustaafu, mwanawe Museveni aonya upinzani

Muhoozi amezua mjadala mpya nchini Uganda kwa kudai kuwa ndiye rais anayefuata wa nchi hiyo.

image
na Radio Jambo

Habari15 October 2022 - 05:10

Muhtasari


•Muhoozi alionyesha imani kuwa upinzani chini ya mwanamuziki aliyegeuka mwanasiasa Robert Kyagulanyi almaarufu Bobi Wine hautawahi kuongoza nchi baada ya kustaafu kwa babake.

•Mnamo Mei 2019, Muhoozi alichapisha meme inayoonyesha jinsi yeye na 'kaka yake' walivyokuwa waking’ang’ania  nafasi hiyo.

KWA HISANI

Mtoto wa Rais Yoweri Museveni Muhoozi Kainerugaba amezua mjadala mpya nchini Uganda kwa kudai kuwa ndiye rais anayefuata wa nchi hiyo.

Muhoozi alionyesha imani kuwa upinzani chini ya mwanamuziki aliyegeuka mwanasiasa Robert Kyagulanyi almaarufu Bobi Wine hautawahi kuongoza nchi baada ya kustaafu kwa babake.

"Kwa upinzani wa Uganda, baada ya baba yangu, nitawashinda vibaya katika uchaguzi wowote. Waganda wananipenda zaidi kuliko watakavyowahi kuwapenda," alisema kupitia Twitter siku ya Ijumaa.

Uganda ifanya uchaguzi mwaka wa 2026 kumchagua rais mpya. Museveni ameiongoza nchi hiyo tangu alipoingia madarakani mwaka 1978.

Bobi Wine, kiongozi wa National Unity Platform, alitangaza azma yake ya urais kwa mara ya kwanza mwaka wa 2019 lakini akashindwa na Museveni katika uchaguzi wa 2021.

Hii si mara ya kwanza kwa Muhoozi kutoa maoni kuhusu mrithi wa urais.

 Mnamo Mei 2019, Muhoozi alichapisha meme inayoonyesha jinsi yeye na 'kaka yake' walivyokuwa waking’ang’ania  nafasi hiyo.

Aliandika, "Mimi na kaka yangu mdogo Kabobi tukibishana kuhusu nani anaweza kujaza viatu vya baba yangu! Shukrani kwa msanii bora nchini Uganda."

Akijibu tweet hiyo Bobi Wine alisema mimi sio kaka yako na wala sishindani na viatu vya baba yako, unastahili viatu vya M7, ng'ombe na hata kofia yake, kosa moja unalofanya ni kudhani Uganda ndio moja ya mali za baba yako ili urithi."

Kiongozi huyo wa upinzani siku za nyuma alidai kuwa Museveni alikuwa akimtayarisha Muhoozi kuwania kiti hicho, kwa nia ya kutaka kumpata mfalme.

Katika jibu la tweet ya Muhoozi siku ya Ijumaa, mtumizi wa Twitter aliuliza ikiwa kwa maneno "baada ya baba yangu", alimaanisha kuitambulisha Uganda kama eneo la ufalme.

"Chochote unachotuita. Uganda kamwe haitakuwa mali ya ukoloni mamboleo," Muhoozi alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved