China inadaiwa kufungua vituo vya polisi nchini Nigeria, Lesotho na Tanzania ili kudhibiti vitendo vya uhalifu vinavyofanywa na raia wake wanaoishi katika nchi hizo tatu za Afrika, tovuti inayomilikiwa na mtu binafsi ya Nigeria ya Vanguard imeripoti.
Wakiwanukuu watetezi wa Usalama, Vanguard imesema mpangilio wa China unaweza kuonekana kama shambulio dhidi ya uhuru wa eneo husika.
"Badala ya kushirikiana na serikali za mataifa hayo, [China] imeamua… kushirikiana na United Front linked , mashirika ambayo yako nje ya nchi katika mabara matano, kuanzisha mfumo mbadala wa polisi na mahakama ndani ya nchi tatu, na kuhusisha moja kwa moja mashirika hayo katika mbinu zisizo halali zinazotumiwa kuwasaka 'wakimbizi'," Watetezi hao wa usalama walisema walisema.
Waliongeza kuwa mamlaka ya China, kati ya Aprili 2021 na Julai 2022, "imewashawishi" raia 230,000 kurejea China kujibu mashtaka ya jinai kuhusu mawasiliano ya simu na ulaghai wa jumla.
Pia ilisema serikali ya China ilipiga marufuku raia wake kuhamia nchi tisa ambazo hazikutajwa kwa makosa ya "udanganyifu mkubwa, ulaghai wa simu na uhalifu wa mtandao".