Marekani yaipatia Ukraine msaada wa kijeshi wa dola milioni 275

Hayo yamesemwa na naibu msemaji wa Ikulu ya Marekani Sabrina Singh katika mkutano fupi.

Image: BBC

Marekani inaipa Ukraine kifurushi kipya cha msaada wa kijeshi kiasi cha dola milioni 275.

Hayo yamesemwa na naibu msemaji wa Ikulu ya Marekani Sabrina Singh katika mkutano fupi.

Kulingana naye, hii ni pamoja na, risasi za ziada kwa mifumo ya roketi ya kurusha ya HIMARS, makombora 500 ya usahihi wa hali ya juu na makombora 2,000 ya RAAMS kwa mizinga 155 mm, makombora 1,300 ya kukabiliana na vifaru, magari 125 ya kijeshi ya Humvee, silaha ndogo ndogo na risasi milioni 2.7 na antena 4 za mawasiliano ya satelaiti.

"Tangu kuanza kwa utawala wa Biden, Marekani imetenga dola bilioni 18.5 kama msaada wa kijeshi kwa Ukraine,"alibainisha.

"Tumepata silaha zaidi za HIMARS, makombora na vifaa vingine. Tunashukuru washirika wetu," alisema mkuu wa ofisi ya rais Andriy Yermak kupitia mtandao wa telegram.