logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kutana na mtu mwenye pua refu duniani

Pua yake inaaminika kuwa ya sentimita 19 ambayo ni inchi 7.5

image
na Radio Jambo

Makala16 November 2022 - 07:40

Muhtasari


• Thomas aikuwa maarufu wakati wa karne ya 18 kutokana na juhudi zake alizozioyesha akijaribu kufaya sarakasi kwenye maonyesho yaliyotazamwa na halaiki ya watu.

Thomas Wedders mwenye pua kubwa ya sentimita 19

Picha ya mwanamume mmoja kutoka Yorkshire nchini Uingereza inazidi kuzua gumzo mitandaoni baada yake kugonga vichwa vya habari  alipotajwa kuwa binadamu mwenye pua refu duniani.

Thomas Wedders  kutoka Uingereza anaripotiwa kuwa na pua yenye urefu wa sentimita 19 ambayo ni inchi 7.5 kwenye chapisho kwenye tovuti ya Guinness World Records.

Baada ya picha ya umbo ya pua yake iliyofanya maelfu ya watumiaji wa mitandao ya kijamii kutoa maoni yao wakichanganyikiwa.

 

Hadithi ya Wedders ilipata ulipata ufuatiliaji mwingi mitandaoni baada ya ukurasa wa Twitter uitwao Historic Vids kuchapisha picha ya pua yake na kusema kuwa ina urefu usio wa kawaida.
 
Alianza kuwa maarufu tangu karne ya 18 kutokana na juhudi zake alizozioyesha kijaribu kufaya sarakasi kwenye maonyesho yaliotazamwa na umati wa watu.
 
Hata hivyo rekodi ya dunia ya mtu mwenye pua kubwa zaidi kuliko ya Wedders ni ya jamaa kwa jina  Mehmet Ozyurek kutoka Uturuki ambaye alivikwa taji hilo mnamo Novemba mwaka 2022 kama mtu mwenye  pua yenye ukubwa wa inchi 3.46.
 
Watumizi wa mitandao walionekana kuachwa vinywa wazi kutokana na kushtushwa na umbile la pua yake. Wengi hawakuamini.
 
Jake mammal alisema, ''Hiyo sio pua. Nimekataa!''

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved