Mamilioni washiriki kura ya maoni kutaka Trump arudishwe Twitter

trump alifungiwa akaunti yake rasmi yenye mamilioni ya wafuasi baada ya kupinga ushindi wa rais Biden miaka miwili iliyopita.

Muhtasari

• Zaidi ya watu asilimia 52 tayari walikuwa wametoa maoni yao kuwa ya ndio dhidi ya asilimia 47 wanaosema hapana.

Mamilioni wapiga kura wakitaka Trump arudishwe Twitter
Mamilioni wapiga kura wakitaka Trump arudishwe Twitter
Image: Maktaba

Tajiri mmiliki mpya wa mtandao wa Twitter, Elon Musk ameandaa kura ya maoni kweney mtandao huo akitaka wafuasi wake na watumizi wa mtandao wa Twitter kwa jumla kutathmini mustakabli wa aliyekuwa rais wa Marekani, Donald Trump mtandaoni hapo.

Musk aliwataka wana Twitter kupiga kura iwapo wanataka Trump kurudishwa Twitter au kuendelea kufungiwa nje ya mtanda ohuo mkubwa kwa watumizi wa kuzungumzia mambo mbali mbali kijamii.

Zaidi ya watu asilimia 52 tayari walikuwa wametoa maoni yao kuwa ya ndio dhidi ya asilimia 47 wanaosema hapana kwa maana kuwa hawataki Trump kurejeshewa uhuru wake wa kuzungumza kupitia Twitter.

Wakati wa uchaguzi wa Marekani, Trump alifungiwa nje ya akaunti yake kwa saa 12 baada ya kuwasifu kwa ushujaa mamia ya wafuasi wake walioingia Ikulu ya Marekani kama Bunge la Marekani na kujaribu kupinga ushindi wa Joe Biden katika uchaguzi wa urais.

Twitter hapo awali ilionya kwamba itapiga marufuku akaunti yake ikiwa atakiuka sheria za jukwaa tena.

Baada ya kuruhusiwa kurudi kwenye Twitter, Trump alichapisha tweets mbili ambazo kampuni hiyo ilizitaja kama za mwisho kutoka kwake.

Tangu hapo, mtandao huo ulimfungia nje kabisa Trump kwa kile walisema kwamba tweets zake zilikuwa za kuchochea ustawi wa Marekani baada ya kuonekana hadharani kutokubali kushindwa na Joe Biden ambaye alikuwa anamuona kama mshindani dhaifu.