Aingia kwenye klabu ya jinsia moja na bunduki, aua 5 na kujeruhi 18 Colorado Marekani

Mtu mmoja aliyekuwa na risasi alishambulia klabu hiyo

Muhtasari

• Hii ni baada ya mtu aliyekuwa na silaha kushambulia kwa risasi klabu ya wapenzi wa jinsia moja.

Image: BBC

Takriban watu watano wameuawa na wengine 18 kujeruhiwa katika jimbo la Colorado nchini Marekani Jumamosi usiku. 

Hii ni baada ya mtu aliyekuwa na silaha kushambulia kwa risasi klabu ya wapenzi wa jinsia moja.

Polisi walisema mshukiwa, kwa jina Anderson Lee Aldrich, 22, amekamatwa na anatibiwa majeraha.

Watu wawili "mashujaa" kwenye kilabu walifanikiwa kumdhibiti mshambuliaji, polisi walisema.

Club Q, huko Colorado Springs, ilitoa taarifa kwenye Facebook ikisema "imehudhunishwa na shambulio lisilo na maana kwa jamii yetu".

Polisi wa Colorado Springs waliwataka watu kuwa na subira wakati wanafanya kazi ya kutambua waathiriwa na kukamilisha idadi ya majeruhi. Mshukiwa huyo alipatikana ndani ya klabu hiyo wakati polisi walipoingia.

Mwaka wa 2016, watu 49 waliuawa na zaidi ya 50 kujeruhiwa kwa risasi kwenye klabu ya usiku ya wapenzi wa jinsia moja huko Orlando, Florida. Kwa wakati huo hayo yalikuwa mauaji mabaya zaidi ya watu wengi kwa wakati mmoja katika historia ya Marekani.