Hofu ya Ebola yafanya Uganda kufunga shule mapema kwa likizo ya Krismasi

Ebola ni maambukizi ya virusi ambayo husambazwa kupitia maji maji ya mwili wa mgonjwa.

Muhtasari
  • Katika miezi miwili iliyopita watu 55 wamekufa na virusi hivyo - na kuna uwezekano wa vifo 22 vya Ebola kabla ya mlipuko huo kutangazwa rasmi mnamo 20 Septemba
Image: BBC

Krismasi huenda inakuja mapema kwa wanafunzi nchini Uganda hukumamilioni yao wakirejea nyumbani mapema kwa likizo ya shule siku ya Ijumaa.

Hata hivyo uamuzi wa kufungwa kwa shule kote nchini wiki mbili kabla ya mwisho wa muhula umechukuliwa ili kuzuia kuenea kwa Ebola, huku nchi hiyo ikiendelea kupambana na moja ya milipuko yake mbaya zaidi.

Pia inakinzana na msimamo rasmi wa serikali kwamba hali imedhibitiwa.

Katika miezi miwili iliyopita watu 55 wamekufa na virusi hivyo - na kuna uwezekano wa vifo 22 vya Ebola kabla ya mlipuko huo kutangazwa rasmi mnamo 20 Septemba.

Baadhi ya wataalam wameelezea kutoridhishwa kwao na hatua ya kufungwa kwa shule, wakisema kuwa kuwaweka wanafunzi ndani kwa wiki nyingine mbili itakuwa njia bora ya kukomesha kuenea kwa ugonjwa huo hatari.

Ebola ni maambukizi ya virusi ambayo husambazwa kupitia maji maji ya mwili wa mgonjwa.