Mtoto wa miaka 5 anusurika kifo kwa kuumwa na chatu akiogelea

Chatu huyo alikuwa wa mita 3, sawa na urefu wa futi 10

Muhtasari

• Chatu alimng'ata mtoto, akatumbukia ndani ya maji na kujifunganisha mguuni mwa mtoto huyo.

•Baba mtoto ndiye aliyekuja haraka na kuogelea na kumwokoa mtoto wake.

Image: kwa hisani

Mtoto wa miaka 5 alinusurika kifo baada ya  kuumwa na kubanwa  na chatu mkubwa baada ya kumwagusha kwenye bwawa la kuogelea huko Sydney, Australia.

Mtoto huyo, Beau  alikuwa akicheza kando ya bwawa hilo wakati ambapo chatu mwenye urefu wa mita 3, sawia na futi 10 alipotokea kwenye mimea iliyokuwa karibu na kumrusha kwenye bwawa hilo chini ya maji.

"Ninaamini chatu alikuwa amekaa pale akingojea mtu aje, ndege au kitu ila Beau ndiye alikuwa karibu." Ben Blake, baba mtoto aliambia vyombo vya habari.

Chatu alimng'ata mtoto, akatumbukia ndani ya maji na kujifunganisha mguuni mwa mtoto huyo.

Babu wa mvulana mwenye umri wa miaka 76 aliingia kwenye uokoaji, akipiga mbizi kwenye bwawa na kumwinua mvulana huyo na kumtoa nje  huku nyoka akiwa bado amemshika.

"Mimi sio kijana mdogo, nilimfanya mtoto wangu aachiliwe  na chatu ndani ya sekunde 15-20," baba aliambia vyombo vya habari.

Baba alielezea tukio hilo kama tukio la ajabu na la taabu kutokea na kuongeza kuwa mvulana huyo sasa anaendelea kupata nafuu.

"Tulishafisha damu na kumwambia mtoto wangu kuwa huyo sio nyoka mwenye sumu,sasa yuko salama," Blake alisema.

Kwa kuwa chatu hawana sumu, mtoto huyo anatibiwa kuzuia matatizo ambayo yangekuja kutokana na kuumwa.

Blake alisema kuwa nyoka huyo aliachiliwa na moja kwa moja akarudi kwenye mimea.

Haya yanajiri baada ya mwili wa mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 50 katika jimbo la Jambi nchini Indonesia kumezwa mzima na chatu.

Mwanamke huyo Jahrah na ambaye alikuwa mcheza mpira, alikuwa ameenda kazini kwenye shamba la miti baada ya kupatana na chatu huyo.

Baada ya kutafutwa kwa mda mrefu mwanamke huyo aligundulika na wanakijiji akiwa ndani ya chatu aliye kuwa na tumbo kubwa. Wenyeji baadaye walimuua nyoka huyo na kupata mwili wake ndani.