Televisheni ya China inadhibiti picha za mashabiki wa Kombe la Dunia wasio na barakoa

Wachina walionyeshwa hisia za makocha badala ya mashabiki wakisherehekea.

Muhtasari

•Jumatatuwakati wa mechi ya Korea Kusini na Ghana, China walihakikisha watazamaji hawakuonyeshwa picha za wafuasi wasio na barakoa.

•Badala ya kuonyeshwa mashabiki wenye mbwembwe, watazamaji wa China waliona hisia za kocha wa Korea Kusini Paulo Bento na meneja wa Ghana Otto Addo.

Picha kama hizi za mashabiki wasio na barakoa hazijaonyeshwa kwa uwazi sana katika utangazaji wa Uchina wa Kombe la Dunia
Picha kama hizi za mashabiki wasio na barakoa hazijaonyeshwa kwa uwazi sana katika utangazaji wa Uchina wa Kombe la Dunia
Image: BBC

Maneno "mpira wa miguu si kitu bila mashabiki" umekubalika na wachambuzi.

Lakini TV ya serikali ya China imekuwa ikijaribu kuukosesha maana msemo huo katika Kombe la Dunia.

Siku ya Jumatatu, Ghana ilipoishinda Korea Kusini katika pambano la kawaida la Kombe la Dunia, kwa upande wa China walihakikisha watazamaji hawakuonyeshwa picha za wafuasi wasio na barakoa – tofauti na kwa ulimwengu unaosonga mbele kutokana na vizuizi vya Covid.

Wale wanaotazama kwenye BBC - na katika sehemu nyingi duniani - watakuwa wameona skrini zao zikijaa picha ya shabiki wa Ghana anayeng’aa, asiye na barakoa akisherehekea kwa furaha huku kamera ikikaribia.

Baada ya Mohammed Kudus kupiga bao la ushindi dakika ya 68, picha za mashabiki wakicheza na kushangilia - pamoja na mashabiki wa Korea Kusini waliokuwa na wasiwasi - ziliangaziwa kote ulimwenguni.

Lakini sio Uchina, ambapo wale wanaotazama kwenye chaneli ya michezo ya shirika la utangazaji la serikali, CCTV 5, watakuwa wanaona nyakati hizi tofauti.

Badala ya kuonyeshwa mashabiki wenye mbwembwe, watazamaji wa China waliona hisia za kocha wa Korea Kusini Paulo Bento na meneja wa Ghana Otto Addo.

Na mchezo ulipofikia tamati, wafuasi wa Korea Kusini waliokuwa wanatiririkwa na machozi wakiwa wameshika vichwa vyao kwa mikononi yao picha hiyo haikuonekana kwenye matokeo ya Uchina.

Wakati maandamano yalitikisa China, watendaji wa Televisheni ya serikali wamekuwa waangalifu kuzuia picha za ulimwengu kuonekana na raia wao kama vile mashabiki wasio kuwa na barakoa.

Sio kawaida kwa watangazaji katika mashindano makubwa kupewa chaguo la kuchagua kamera zao zitakako kuwa, na mara nyingi pia huchelewesha kidogo picha zao ili kuruhusu uhariri na uteuzi wa picha kabla ya umma kuziona.

BBC iliona kuwa kulikuwa na kuchelewa katika uonyesha wa matangazo ya moja kwa moja kwa takribani sekunde 52 kati ya utangazaji wake na CCTV 5.