Haijawahi niingia akilini kutaka kuwa rais wa Uganda - Muhoozi Kainerugaba

imi tayari ni kiongozi wa kizazi changu! Hiyo ndiyo heshima kubwa zaidi ninayoweza kufikiria - Alisema.

Muhtasari

• Baada ya wiki chache, nitatoa tangazo muhimu. Sio kwenye Twitter lakini kwa njia zingine - alisema.

KWA HISANI
KWA HISANI
Image: Muhoozi Kainerugaba

Muhoozi Kainerugaba, mkuu wa majeshi ya Uganda ambaye pia ni mtoto wa rais Yoweri Museveni amenyoosha maelezo kuwa hata siku moja hajawahi kufikiria mambo ya kuwania urais wa Uganda.

Matamshi haya yake kupitia Twitter yanakuja wakati ambapo wengi wamekuwa wakiibua maneno kuwa Museveni ana njama ya kumuandaa Muhoozi kuwa mrithi wake pindi atakapostaafu kuelekea uchaguzi mkuu ujao mwaka 2024.

Muhoozi alikanusha hayo na kusema kuwa yeye kwa sasa ni mkuu wa kamanda wa majesho ya Uganda, nafasi ambayo ni ya juu kabisa katika maisha yake na anafurahia hilo na kujivunia pia.

“Kuna watu wanaendelea kusema nataka kuwa Rais? Kusema ukweli hilo halijawahi kuwa akilini mwangu. Mimi tayari ni kiongozi wa kizazi changu! Hiyo ndiyo heshima kubwa zaidi ninayoweza kufikiria. Kizazi chetu kitakuwa kikubwa zaidi!!” Kainerugaba alitweet.

Lakini aliwataka wote ambao wanataka awe mrithi wa baba yake kuretweet kama watakuwa wengi basi atafikiria upya.

“Sawa, waache wanaotaka niwe Rais baada ya baba ku-tweet na kulike. Ukinishawishi nitafanya.”

Alisema kuwa wiki chache zijazo atatoa tangazo la kutingiza ardhi, ambalo litatoa mwelekeo sawia wa kisiasa kwa vijana wa kizazi chake.

“Baada ya wiki chache, nitatoa tangazo muhimu. Sio kwenye Twitter lakini kwa njia zingine. Nitafanikiwa kwa uwezo wangu binafsi na kama kiongozi wa kizazi chetu,” Kainerugaba alitweet.