Facebook kutoa uamuzi iwapo akaunti ya Donald Trump itarudishwa

Hatua hii inakuja miezi michache baada ya Twitter kurudisha akaunti ya rais huyo wa 45 wa Marekani.

Muhtasari

• Trump alipigwa marufuku kutoka kwa majukwaa ya Meta ya Facebook na Instagram baada ya shambulio la Ikulu ya Marekani mnamo Januari 2021.

• Iwapo ataruhusiwa kurejea Facebook, utakuwa ni msukum mkubwa kwa kampeni zake za urais wa 2024 ambao ametangaza kuwania.

Facebook kutathmni kurudisha Trump
Facebook kutathmni kurudisha Trump
Image: Maktaba, Wikipedia

Mamlaka ya Facebook iliyoko chini ya mwavuli wa Meta imetangaza kuwa inatathmini iwapo itarudisha akaunti ya aliyekuwa rais wa 45 wa Marekani, Donald Trump.

Kulingana na CNN, Facebook ilisema kuwa katika wiki chache zijazo, itatoa tamko kuhusu uamuzi wa kurejeshwa kwa akaunto hiyo kwenye mtandao huo, miaka miwili tangu ilipofungwa katika kile Facebook walisema ni ukiukwaji wa maadili ya jamii ya watumizi wa Facebook.

Uamuzi huo, ambao unaweza kuwa muhimu zaidi katika historia ya kampuni, unazingatiwa na kikundi maalum cha wafanyikazi wa kampuni inayoundwa na viongozi kutoka sehemu tofauti za shirika la Meta.

Trump alipigwa marufuku kutoka kwa majukwaa ya Meta ya Facebook na Instagram baada ya shambulio la Ikulu ya Marekani mnamo Januari 2021. Hapo awali, marufuku hiyo ilikuwa ya muda usiojulikana, lakini hiyo ilirekebishwa baadaye, na kampuni hiyo ilisema ingezingatia kumruhusu Trump kurudi kwenye majukwaa baada ya miaka miwili. Miaka hiyo miwili inapita Jumamosi, Januari 7, 2023.

Hapo awali Meta ilisema Trump alifungiwa kwenye majukwaa yake kutokana na kuwasifia watu waliohusika katika vurugu katika Ikulu ya Marekani.

Tangazo hili linajiri miezi michache tu baada ya Twitter kumrudishia Trumo akaunti yake kufuatia kura ya maoni ambayo mmiliki mpya wa mtandao huo Elon Musk aliweka na wengi wakapiga kura kutaka Trumo kurudishwa Twitter.

Iwapo Facebook wataafikiana kumrudisha Trump kwenye jukwaa hilo ,hiyo itakuwa hatua kubwa sana kwa upande wake na italeta msukumo wa aina yake katika kampeni za urais wa mwaka 2024 ambapo tayari Trump ametangaza kuwania tena baada ya kushindwa katika uchauzi wa 2020 na rais wa sasa Joe Biden.