Takribani watu 68 wafariki baada ya ndege kuanguka Nepal

Manusura kadhaa waliojeruhiwa vibaya walipelekwa hospitalini.

Muhtasari

•Ndege iliyokuwa na watu 72 imeanguka karibu na uwanja wa ndege katikati mwa Nepal na takriban miili 40 imepatikana,

Image: BBC

Takriban watu 68 wamethibitishwa kufariki, baada ya ndege kuanguka Nepal, maafisa walisema.

Manusura kadhaa waliojeruhiwa vibaya walipelekwa hospitalini, ripoti ambazo hazijathibitishwa zilisema.

 maafisa wanasema.

Ndege ya shirika la ndege la Yeti kutoka Kathmandu kuelekea mji wa kitalii wa Pokhara ilianguka wakati ikitua na kushika moto.

Video zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonesha ndege ikiruka chini chini kwenye eneo lenye watu wengi kabla ya kuzunguka kwa kasi.

Kulikuwa na abiria 68 ndani ya ndege hiyo, wakiwemo takribani raia 15 wa kigeni na wafanyakazi wanne.

Ajali za ndege si za kawaida nchini Nepal, mara nyingi kutokana na njia zake za kukimbia zilizo mbali na mabadiliko ya ghafla ya hali ya hewa ambayo yanaweza kuleta hali ya hatari.

Ndege ya Tara Air ilianguka Mei 2022 katika wilaya ya kaskazini mwa Nepal ya Mustang, na kuua watu 22.

Mwanzoni mwa mwaka wa 2018, watu 51 walipoteza maisha wakati ndege ya US-Bangla iliyokuwa ikisafiri kutoka Dhaka nchini Bangladesh iliposhika moto ilipokuwa ikitua Kathmandu.