DRC: ''Rwanda imedungua ndege yetu ya kivita ikiwa katika anga la DRC, Tutajibu''

Rwanda imeionya DRC kukomesha kitendo hicho ilichotaja kuwa cha uchokozi.

Muhtasari

•Kinshasa iliita tukio hilo "uchokozi" na kusema ingawa inakaa katika michakato ya amani "ina haki halali ya kutetea eneo lake na haitaiacha".

•Kuna Picha zilizoonekana za ndege hiyo ikimwagiwa vizima moto katika uwanja wa ndege wa Goma, huku baadhi ya sehemu zake zikiwa zimeharibika.

Image: BBC

Taarifa ya serikali ya DRC "imelaani shambulizi" kwenye ndege yake ya kivita iliyopigwa kombora na "na jeshi la Rwanda" wakati ikitua kwenye uwanja wa ndege wa Goma "ikiruka katika ardhi ya Congo".

Kinshasa iliita tukio hilo "uchokozi" na kusema ingawa inakaa katika michakato ya amani "ina haki halali ya kutetea eneo lake na haitaiacha".

Awali, Serikali ya Rwanda ilitangaza kwamba "hatua za usalama zimechukuliwa" dhidi ya ndege ya kivita ya DR Congo ya Sukhoi-25 ambayo Rwanda imesema iliingia kwenye anga ya Rwanda kwa mara ya tatu" jana jioni.

Rwanda imeionya DRC kukomesha kitendo hicho ilichotaja kuwa cha uchokozi.

Tukio hilo ni mzozo wa hivi karibuni kati ya nchi hizo mbili ambazo uhusiano wao unazidi kuzorota kutokana na madai kutoka kila nchi ya uungwaji mkono makundi ya waasi.

Video iliyosambazwa sana kwenye mitandao ya kijamii ilionesha kombora likifwata ndege ya kijeshi angani na kuipiga bila kuiangusha. Baadhi ya watu walioshuhudia wanasema kuwa ndege hii ilikuwa katika anga ya mjini Goma nchini DRC, wengine walisema ilikuwa katika anga ya mjini Rubavu nchini Rwanda, hii ni miji inayopakana sana.

Kuna Picha zilizoonekana za ndege hiyo ikimwagiwa vizima moto katika uwanja wa ndege wa Goma, huku baadhi ya sehemu zake zikiwa zimeharibika.

Tangazo la serikali ya Rwanda limeonya nchi ya Jamuhuri ya kideomkrasia ya Congo kukomesha kile ambacho serikali ya Rwanda imetaja kuwa uchokozi. Mnamo Novemba mwaka jana , Rwanda ilisema kuwa ndege ya DR Congo ya Sukhoi-25 iliingia kwenye anga yake, ambapo DRC ilisema ilikuwa ni kwa bahati mbaya.

Jana Jumanne, mapigano makali yalitokea kati ya waasi wa M23 na wanajeshi wa serikali ya DR Congo katika maeneo tofauti ya Rutshuru karibu na Masisi.

Tukio hilo ni mzozo wa hivi karibuni kati ya nchi hizo mbili ambazo uhusiano wao unazidi kuzorota kutokana madai kutoka kila upande ya uungwaji mkono makundi ya waasi.

Kinshasa inaishutumu Kigali kwa kuwasaidia waasi wa M23 kwa kuwapa wanajeshi na silaha, Kigali inasema haina uhusiano wowote na M23 na kuishutumu DRC kushirikiana na waasi kutoka Rwanda wa FDLR.