Rashid Simai Msakara, mkuu wa wilaya ya mjini Magharibi Unguja amepiga marufuku midoli ya kuvishwa nguo kuonesha nje ya maduka hayo ya kuuza nguo katika wilaya yake.
Kulingana na taarifa kutoka nchini Tanzania, mkuu wa wilaya alisema midoli hiyo inavishwa nguo zisizo na stara na kuoneshwa nje kama njia moja ya kuwavutia wanunuzi, jambo alilolitaja kuwa lisilo sahihi.
DC Msaraka alitoa kauli hiyo baada ya kukutana na Mfanyabiashara maeneo ya Zanzibar akiwa ameweka midoli hiyo nje ya duka ikiwa imevalishwa nguo ambazo zinadaiwa kupotosha maadili ya Zanzibar hususani kwa Watoto pindi wanapoona midoli hiyo imevishwa nguo hizo.
DC Msaraka alisema kuwa maarufuku hiyo imetokana na Watoto na Vijana kuona vitu visivyo na staha na kupelekea kuvuraga akili za Vijana wa Zanzibar.
“Maelekezo yangu hapa yatafuata maelezo kuhusu hivi vitu. Kwa sasa hatutaki. Weka biashara yako ndani, kwanza yenyewe hii kuweka nje ni marufuku hata kama ni hizo nguo za kawaida. Kwa leseni yako inakuelekeza uweke biashara yako ndani, sio nje. Hii ondoa kinyume chake tutachukua hatua. Kwanza hii inaharibu utaratibu,” DC huyo alimfokea mfanyibiashara huyo.
Hata hivyo, alisema kwamba agizo hilo linamaanisha kupiga marufuku nguo hizo kwani yeyote anayetaka kuzinunua ana uhuru wake kuzinunua, ila matangazo yake kupitia midoli hiyo yasiwekwe nje hadharani.
“Kwa anaye taka kununua nguo hizi hatumkatazi, na anunua avae, huo ni uhuru wake mwenyewe atajua yeye mwenyewe ataivaa wapi na kwa utaratibu upi. Wewe unayeagiza usiweke nje. Leo hii nitatoa tangazo kwa wilaya ya mjini yote ni marufuku kuweka midoli yenye midoli zisizo kuwa za staha nje, ni marufuku,” DC huyo alisema.