logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwanajeshi wa Marekani abubujikwa na machozi akielezea aliyopitia Afghanistan

Wanajeshi 13 wa Marekani waliuawa katika shambulio hilo la bomu, pamoja na raia 170 wa Afghanistan.

image
na Radio Jambo

Makala09 March 2023 - 03:45

Muhtasari


•Tyler alielezea kuwa kulikuwa na kipindi cha machafuko na kutojiandaa siku kadhaa baada ya Taliban kuteka Kabul.

•Wanajeshi 13 wa Marekani waliuawa katika shambulio hilo la bomu, pamoja na raia 170 wa Afghanistan.

•Alielezea wakati wa shambulio la bomu, yeye alifumba macho na kufungua akaona wenzake wamekufa au wamelala karibu naye bila kujitambua.

Askari wa zamani wa majini wa Marekani aliyejeruhiwa vibaya nchini Afghanistan ameelezea kujiondoa kwa nchi yake mwaka 2021 kuwa ni "janga" katika ushahidi mbele ya bunge.

Tyler Vargas-Andrews amezungumza kwa mara ya kwanza katika mkutano ulioongozwa na Republican wa kuchunguza jinsi utawala wa Biden ulivyoshughulikia kuondolewa kwa wanajeshi nchini Afghanstan.

Alielezea kuwa kulikuwa na kipindi cha machafuko na kutojiandaa siku kadhaa baada ya Taliban kuteka Kabul.

Wengine walizungumza juu ya kuvumilia kiwewe na maumivu waliyopata baada ya matokeo.

Sgt Vargas-Andrews, 25, alikuwa mmoja wa wanajeshi kadhaa wa Marekani waliopewa jukumu la kulinda uwanja wa ndege wa Kabul mnamo tarehe 26 Agosti 2021, wakati washambuliaji wawili wa kujitoa mhanga waliposhambulia umati wa Waafghanistan wakijaribu kuwakimbia Taliban wakati wa uhamisho wa Marekani.

Wanajeshi 13 wa Marekani waliuawa katika shambulio hilo la bomu, pamoja na raia 170 wa Afghanistan.

Sgt Vargas-Andrews alitoa ushahidi kwamba yeye na mwanajeshi mwingine walipokea taarifa za kijasusi kuhusu shambulio hilo kabla halijatokea, na kwamba alimwona mshukiwa kwenye umati.

Alisema aliwatahadharisha wasimamizi wake na kuomba kibali cha kuchukua hatua lakini hakupata ruhusa. "Tulipuuzwa kirahisi tu," Sgt Vargas-Andrews alisema.

Akitoa ushuhuda kwa hisia kali, alielezea wakati wa shambulio la bomu ambalo lilirushwa hewani na yeye alifumba macho na kufungua akaona wenzake wamekufa au wamelala karibu naye bila kujitambua.

"Mwili wangu ulizidiwa kutokana na kiwewe cha mlipuko huo. Tumbo langu lilikuwa limepasuliwa. alisema. Sgt Vargas-Andrews na kuuita uondoaji huo kuwa "janga," na kuongeza: "Kulikuwa na ukosefu usio na sababu wa uwajibikaji na uzembe."


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved