Rais wa Sudan Kusini amfukuza kazi waziri wa mambo ya nje

Waziri huyo aliyefutwa kazi ni mshirika wa Bw Kiir, na hapo awali aliwahi kuwa waziri katika ofisi ya rais.

Muhtasari
  • Kufutwa kazi kwao kumetishia kuvuruga makubaliano ya amani na kiongozi wa upinzani Makamu wa Kwanza wa Rais Riek Machar
RAIS WA SUDAN KUSINI KIIR
Image: KWA HISANI

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amemfuta kazi waziri wake wa mambo ya nje, baada ya kuwafuta kazi mawaziri wa ulinzi na mambo ya ndani katika kipindi cha wiki moja.

Hakuna maelezo yaliyotolewa kuwa sababu ya kufukuzwa kazi kwa Mayiik Ayii Deng, ambayo ilitajwa katika matangazo ya runinga ya serikali.

Waziri huyo aliyefutwa kazi ni mshirika wa Bw Kiir, na hapo awali aliwahi kuwa waziri katika ofisi ya rais.

Kufutwa kazi kwao kumetishia kuvuruga makubaliano ya amani na kiongozi wa upinzani Makamu wa Kwanza wa Rais Riek Machar.

Upinzani ulitoa wito wa kurejeshwa kwa Angelina Teny, ambaye Bw Kiir alimfukuza kama waziri wa ulinzi na kukabidhi nafasi hiyo kwa chama chake. Bi Teny pia ni mke wa Bw Machar.

Umoja wa Mataifa ulitoa wito kwa pande husika "kujizuia na kujihusisha katika hali ya ushirikiano ili kutatua masuala nyeti kama haya ya kitaifa".