Kanisa Katoliki latangaza misa ya kumuombea hayati Magufuli, aliyekuwa rais wa TZ

Magufuli alifariki Machi 2021 miezi michache baada ya kushinda urais kwa mhula wa pili.

Muhtasari

• “Ni miaka miwili tangu kufariki kwake na tunapoendelea kumuombea mpendwa wetu apumzike kwa Amani" sehemu ya tarifa hiyo kwa umma ilisoma.

Kanisa aktoliki yatangaza misa ya kumuombea Magufuli.
Kanisa aktoliki yatangaza misa ya kumuombea Magufuli.
Image: BBC NEWS

Kanisa katoliki katika mkoa wa Mwanza nchini Tanzania limetangaza tarehe ya misa ya kumuombea aliyekuwa rais wa awamu ya tano wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati John Pombe Magufuli.

Katika taarifa iliyotolewa kwa umma wikendo mwishoni mwa juma lililopita, dayosisi kuu ya Mwanza chini ya Askfo Mkuu Renatus Nkwande, aliwaalika Waumini wote kujumuika nao katika misa takatifu itakayofanyika tarehe 25 Machi mwaka huu katika uwanja wa Madhabahu ya Bikra Maria wa Kawekano kuanzia saa nne asubuhi.

“Ni miaka miwili tangu kufariki kwake na tunapoendelea kumuombea mpendwa wetu apumzike kwa Amani, tukumbuke kati ya vitu alivyohimiza ni uzalendo wa dhati, kudumisha Amani, na maendeleo ya taifa kwa jumla,” sehemu ya taarifa hiyo ilisoma.

Magufuli alifariki dunia mnamo Machi tarehe 17 mwaka 2021, miezi michache tu baada ya kushinda uchaguzi wa mwaka 2020 kama rais kwa muhula wa pili.

Kipindi hicho, ulimwengu ulikuwa unapambana jino na ukucha dhidi ya janga la Korona, tatizo ambalo Magufuli alilikemea vikali haswa kwa msimamo wake mkali dhidi ya dawa za kudhibiti msambao wake ikiwemo pia kuweka mikakati ya kudhibiti kusambaa kwa Korona kama uvaaji barakoa na umbali wa kimwili wa mita mbili katika mikusanyiko ya hadhara.

Kifo chake kiliwaliza Watanzania wengi ambao walikuwa wanamuenzi rais huyo kama ‘Jembe’ kwa miradi yake mingi aliyoizindua pamoja na kuwa na msimamo mkali katika kutumbua majipu ya ufisaid kwenye swerikali yake.