Waasi nchini Congo wawaua watu 19

Hili linakuja siku chache baada ya watu 40 kuuawa hivi majuzi.

Muhtasari

•Mashambulizi ya ADF yameua makumi ya watu katika vijiji kadhaa vya Kivu Kaskazini katika siku za hivi karibuni. Mamlaka ya Kongo inasema watu walichinjwa kwa bunduki, visu na mapanga.

Waasi mashariki mwa Kongo waliwaua takriban watu 19 na kuchoma moto kituo cha afya na nyumba, mamlaka iliripoti Jumapili.

Watu wenye silaha wanaoshukiwa kuwa sehemu ya Allied Democratic Forces, wanamgambo wenye uhusiano na kundi la Islamic State, waliwashambulia raia katika mji wa Kirindera, Carly Nzanzu, gavana wa zamani wa jimbo la Kivu Kaskazini, alisema katika mahojiano na vyombo vya habari vya serikali.

Mashambulizi ya ADF yameua makumi ya watu katika vijiji kadhaa vya Kivu Kaskazini katika siku za hivi karibuni. Mamlaka ya Kongo inasema watu walichinjwa kwa bunduki, visu na mapanga.

Aamaq, shirika la habari linalohusishwa na kundi la Islamic State, lilichapisha taarifa Jumamosi ambapo IS ilidai kuhusika na kuwauwa zaidi ya "Wakristo" 35 na kuwajeruhi makumi mashariki mwa Kongo wiki iliyopita.

Migogoro imetanda kwa miongo kadhaa mashariki mwa Kongo, ambapo zaidi ya makundi 120 yenye silaha yanapigania mamlaka, ushawishi na rasilimali, na baadhi kulinda jamii zao. ADF imekuwa ikifanya kazi kwa kiasi kikubwa katika jimbo la Kivu Kaskazini lakini hivi karibuni ilipanua shughuli zake hadi katika jimbo jirani la Ituri. Katuni za Kisiasa za Viongozi wa Dunia