logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mbunge mwanablogu afukuzwa kazini kwa kutohudhuria vikao vya bunge

Mbunge huyo wa miaka 51 alitakiwa kuhudhuria kikao cha kuomba radhi lakini pia hakuhudhuria.

image
na Radio Jambo

Makala16 March 2023 - 06:08

Muhtasari


• Mwanablogu huyo wa YouTube alichaguliwa kama mbunge katika uchaguzi wa mwaka jana Julai lakini hajawahi onekana bungeni.

• Inasemekana kwamba amekuwa uhamishoni Dubai kwa woga kwamba atakamatwa kwa kukashifu serikali.

Mbnge wa Japan afukuzwa kazini kwa kublogi na kuacha kufika bungeni.

Bunge la nchini Japan limemfukuza bungeni mbunge mmoja ambaye pia ni mwanablogu wa YouTube kwa kutohudhuria vikao vya bunge kwa muda mrefu.

Kulingana na jarida la AFP, hii ni mara ya kwanza kwa bunge la taifa hilo la bara Asia kufanya hivyo kwa Zaidi ya miaka 70 iliyopita.

Yoshikazu Higashitani, anayejulikana kwa jina lake la mtandaoni kama GaaSyy, alikuwa ameagizwa kuomba msamaha kwa kutokuwepo kwake kwa miezi kadhaa mapema Machi.

Lakini mbunge huyo, mmoja wa wanachama wawili waliochaguliwa wa chama pinzani Seijika Joshi 48, hakuhudhuria kikao hicho cha bunge pia.

Higashitani, 51, alikuwa hajatia mguu katika Baraza la Madiwani tangu uchaguzi wake wa Julai 2022, licha ya hitaji la wabunge kuwepo.

Mfanyabiashara huyo wa zamani na YouTuber badala yake amesalia nyumbani kwake huko Dubai, akidai huenda akakamatwa ikiwa atarejea Japani, ambako inasemekana anakabiliwa na maswali kuhusu madai ya kukashifu, AFP walieleza.

Baraza la Upper House la Japan liliamua Jumanne kumfukuza kutoka bungeni.

Hatua hiyo ilifanywa rasmi Jumatano -- na kumfanya kuwa mbunge wa kwanza wa Kijapani kufukuzwa tangu 1951, vyombo vya habari vya ndani viliripoti.

Nafasi ya Higashitani itachukuliwa na mwanachama mwingine wa chama chake.

Toleo moja la Seijika Joshi 48 linafanya kampeni za mabadiliko kwa shirika la utangazaji la umma la Japan na hapo awali lilijulikana kama Chama cha NHK.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved