Kampuni ya filamu za watu wazima, MindGeek yanunuliwa na mmiliki wa Canada

Kampuni hiyo imekuwa ikishtumiwa kwa kuonyesha video zenye wahusika watoto na pia maudhui ya ubakaji.

Muhtasari

• Kampuni hiyo imekuwa ikituhumiwa kwa kuendesha maudhui ya filamu za mapenzi yanayowahusisha watoto pamoja pia na ubakaji.

Kampuni ya Kanada yanunua mtandao wa filamu za watu wazima.
Kampuni ya Kanada yanunua mtandao wa filamu za watu wazima.
Image: BBC NEWS

Kampuni moja ya kibinafsi ya Kanada Ethical Capital Partners  siku ya Alhamisi ilitangaza kununua kampuni ya MindGeek ambayo inaendesha tovuti kubwa zaidi ya filamu za watu wazima duniani, jarida la AFP liliripoti.

Masharti ya maafikiano hayajafichuliwa.

MindGeek, ambayo ina makao yake makuu huko Luxembourg ingawa ofisi yake  kubwa iko Montreal, imekuwa ikilengwa katika kesi kadhaa ikidai ilifaidika kutokana na usambazaji wa filamu za mapenzi zinazohusisha watoto bila ridhaa – madai ambayo imekanusha.

Ilianzishwa mwaka 2004, MindGeek inaendesha jalada kubwa la tovuti za burudani za watu wazima, ikijumuisha tovuti mbalimbali maarufu zinazopakia video za watu wazima.

Tovuti hiyo inayoongoza katika soko la filamu za watu wazima kwenye mtandao, hata hivyo, amekabiliwa na msukosuko mkubwa tangu gazeti la New York Times mnamo Desemba 2020 lichapishe makala ambayo tovuti hiyo ilishutumiwa kwa kuchapisha maudhui haramu mtandaoni, zikiwemo video za watoto na video za ubakaji, AFP walieleza.

Hilo lilipelekea wabunge wa Kanada kuwaeleza maafisa wake wakuu kuhusu madai ya unyanyasaji, huku Mastercard na Visa zikisimamisha malipo kwenye tovuti hiyo. Maafisa hao walijiuzulu mnamo Juni 2022.

"Tunashirikiana na timu ya MindGeek na wadau, ikiwa ni pamoja na waundaji wa maudhui, watetezi, watekelezaji wa sheria, washirika wa mashirika ya kiraia na watunga sera ili kufahamisha juhudi zetu na kuimarisha majukwaa salama ya MindGeek, kwenda zaidi ya majukumu ya kisheria na udhibiti,"  Solomon Friedman, mwanzilishi. mshirika wa ECP yenye makao yake makuu Ottawa, alisema katika taarifa kulingana na jarida hilo.