Comrades 50 wadukua mfumo wa karo chuoni na kubadilisha taarifa zao za karo, mitihani

Chuo hicho kilisema wanafunzi zaidi ya 300 walijibadilishia taarifa zao za kifedha kwenye mfumo wa chuo lakini 50 hao walikataa kukiri kupelekea kufukuzwa kabisa.

Muhtasari

• Makamu mkuu wa chuo hicho Profesa Urio aliwaambia waandishi wa habari kuwa uongozi ulibaini kuwa zaidi ya wanafunzi 300 walikuwa wamejibadilishia taarifa zao za karo.

Chuo kikuu cha Iringa chakiri wanafunzi wake wa IT walidukua mfumo wa ada na kujibadilishia taarifa za kifedha.
Chuo kikuu cha Iringa chakiri wanafunzi wake wa IT walidukua mfumo wa ada na kujibadilishia taarifa za kifedha.
Image: Facebook

Wanafunzi wapatao hamsini kutoka chuo kikuu cha Iringa nchini Tanzania ambacho awali kilikuwa kinajulikana kama chuo cha Tumaini wamefukuzwa chuoni na masomo yao kufutiliwa mbali na uongozi wa chuo baada ya kudukua mfumo wa kulipa karo chuoni humo.

Kulingana na taarifa kutoka runinga ya Globla Online nchini humo, hamsini hao walikuwa wote ni wanafunzi wa masomo ya utaalamu wa kimawasiliano na mifumo ya Kielektroniki (IT) na walishirikiana kwa kikoa kudua mfumo huo.

Baada ya kudukua mfumo wa kulipa karo kwa wanafunzi wa chuo hicho, wanafunzi hao watoro walijibadilishia taarifa zao za ada, kila mmoja akijijazia kuwa amekamilisha kulipa karo hali ya kuwa walikuwa na madeni.

Kando na kujibadilishia taarifa zao za kifedha katika mfumo wa chuo, makamu mkuu wa chuo hicho Profesa Urio aliwaambia waandishi wa habari kuwa uongozi ulibaini kuwa zaidi ya wanafunzi 300 pia, walikuwa wamejibadilishia taarifa zao katika mfumo wa ada na kuonekana kuwa wamelipa wakati hawajafanya hivyo.

Aliongeza kuwa baada ya kubaini tatizo hilo, waliwahoji wanachuo hao ambapo 256 kati yao, walikiri kufanya kosa na kuomba msamaha lakini pia wakakubali kulipa kiwango sahihi ambapo wengine 50, waligoma kufanya hivyo na kusababisha wafukuzwe chuoni hapo.

 

Katika taarifa zinazofungamana na udukuzi, serikali ya Kenya mapema jana ilijitokeza na kupinga vikali ufichuzi uliofanywa na Reuters kwamba Uchina ilikuwa imedukua mfumo wake na kupata nyaraka zenye taarifa kuhusu deni la Kenya kwa Uchina.

 

Katibu wa kudumu katika wizara ya usalama wa ndani Raymond Omollo alikanusha taarifa hizo za Reuters akisema kuwa zilinuia kusarambatisha udiplomasia baina ya mataifa hayo mawili na kusema kuwa Uchina haingeweza kudukua mifumo hiyo ambayo mingi yao ni wao walisaidia kuiunda.