logo

NOW ON AIR

Listen in Live

'Landlord' afunga jengo la hospitali ikiwa na wagonjwa ndani akidai kodi milioni 66 - video

Hospitali ya Kimataifa ya Medipal, imekuwa ikifanya kazi katikati mwa Kampala kwa miaka kadhaa.

image
na Radio Jambo

Makala30 May 2023 - 12:23

Muhtasari


• Baadhi walilaumu kitendo hicho kwa hali ngumu ya maisha wakisema kuwa mpaka kufikia hatua hiyo, mmiliki alikuwa amewavumilia hospitali hiyo kwa muda mrefu.

• “Wamekuwa na subira ya hospitali. Ndio maana hata walinzi kuuana kwa sababu ya umasikini.” Mmoja alisema.

Hospitali ya Medipal ilifungwa na Landlord baada ya kushindwa kulipa kodi.

Kizaazaa kilishuhudiwa katika hospitali moja nchini Uganda baada ya mmiliki wa jingo lililokuwa likitumika kama hospitali ya kibinafsi kulifunga wagonjwa wakiwa ndani akidai malimbikizi ya malipo ya kodi.

Kwa mujibu wa video ambayo ilipakiwa na jarida la Daily Monitor, mmiliki kwa jina Temple Steels Uganda LTD aliwatuma walinzi wa kampuni ya Securex kulifunga jingo hilo lililokodishwa na mmiliki wa hospitali ya Medipal International Hospital katika kile alisema kuwa ni kutolipwa malimbikizi ya kodi ambayo yamerundikana hadi shilingi bilioni 1.8 za Uganda, sawa na milioni 66 za Kenya tangu mwezi Septemba mwaka jana.

“Walinzi wa Securex wameacha sehemu moja tu ya kuingia na kutoka kwa wagonjwa na matabibu katika kituo hicho,” sehemu ya ripoti hiyo ilisoma.

Wafanyakazi wa kituo hicho walilazimika kuacha kazi mapema kwa siku hiyo na kuwaacha katika hali tata wagonjwa ambao walikuwa bado wanahitaji huduma za matibabu.

Hospitali ya Kimataifa ya Medipal, taasisi inayomilikiwa na watu binafsi, imekuwa ikifanya kazi katikati mwa Kampala kwa miaka kadhaa.

Baadhi walilaumu kitendo hicho kwa hali ngumu ya maisha wakisema kuwa mpaka kufikia hatua hiyo, mmiliki alikuwa amewavumilia hospitali hiyo kwa muda mrefu.

“Wamekuwa na subira ya hospitali. Ndio maana hata walinzi kuuana kwa sababu ya umasikini.” Mmoja alisema.

Ikumbukwe mapema mwezi huu mlinzi mmoja alimshambulia waziri wa leba na kumuua kwa risasi huku pia walinzi wengine wakizozana na mmoja kumuua mwenzake ndani ya chumba walichokuwa wamepangishiwa na mwajiri wao.

Hii hapa ni video iliyonasa tukio hilo:

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved