logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Marekani yafutilia mbali viza ya Spika wa Bunge la Uganda kuhusu sheria dhidi ya mapenzi ya jinsia moja

Among alikuwa ameweka wazi kwamba "Bunge litasimamia na kuendeleza maslahi ya watu wa Uganda daima."

image
na Radio Jambo

Yanayojiri30 May 2023 - 03:47

Muhtasari


•"Serikali ya Marekani imebatilisha viza yako (Among) ya sasa kuhusu taarifa zilizopatikana baada ya kutolewa kwako mara ya mwisho," Basalirwa alisema.

Marekani imefutilia mbali visa vya Spika wa Bunge la Uganda, Anita Among huku mbunge Asuman Basalirwa akisema yeye ndiye mwathirika wa kwanza wa uwezekano wa kuwekewa vikwazo baada ya taifa hilo la Afrika Mashariki kuhalalisha sheria dhidi ya wapenzi wa jinsia moja , LGBTQ.

"Viza ya sasa ya spika imefutwa na hii inathibitishwa katika barua pepe," Basalirwa ambaye aliwasilisha Mswada huo alisema.

Akinukuu barua pepe hiyo muda mfupi baada ya kujulikana kuwa Rais Museveni alipuuzilia mbali shinikizo la nchi za Magharibi na mashirika ya kutetea haki za binadamu kusaini Mswada wa kupinga mapenzi ya jinsia moja kuwa sheria, Basalirwa aliongeza kuwa:

"Serikali ya Marekani imebatilisha viza yako (Among) ya sasa kuhusu taarifa zilizopatikana baada ya kutolewa kwako mara ya mwisho," alisema alipokuwa akionyesha chapisho la barua hiyo kwa waandishi wa habari Bungeni.

"Kuanzia Mei 12, 2023, wewe (Among) huna viza halali ya Marekani ingawa unakaribishwa kutuma ombi tena," alisema alipokuwa akionyesha chapisho la barua hiyo kwa wanahabari bungeni.

Kulingana na Basalirwa, spika amehimizwa kupeleka paspoti yake kwa Ubalozi wa Marekani kupitia wizara ya fedha kwa ajili ya marekebisho muhimu ya viza yake.

"Nadhani walikuwa wanatafuta visa yangu ya Marekani lakini hawakuipata.Kwa hivyo, mwathiriwa wa kwanza ni spika,” Mbunge huyo wa Manispaa ya Bugiri aliona.

Chini ya sheria mpya, wale wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja wanakabiliwa na adhabu kali ambazo zinaweza kujumuisha kifungo cha maisha.

Mapema Jumatatu, Among alikuwa ameweka wazi kwamba "Bunge litasimamia na kuendeleza maslahi ya watu wa Uganda daima."


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved