Mwanamke aliyewahi kutajwa kuwa "muuaji mbaya zaidi wa kike nchini Australia" amesamehewa baada ya ushahidi mpya kupendekeza kwamba hakuwaua watoto wake wanne wachanga .
Kathleen Folbigg alikaa gerezani kwa miaka 20 baada ya mahakama kugundua kuwa aliwaua Caleb, Patrick, Sarah na Laura kwa zaidi ya muongo mmoja.
Lakini uchunguzi wa hivi majuzi ulishuhudia wanasayansi wakiamini kuwa wanaweza kuwa walikufa kwa njia za kawaida.
Kesi ya mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 55 imetajwa kuwa mojawapo ya makosa makubwa zaidi ya haki nchini Australia.
Bi Folbigg amekuwa akishikilia kwamba hana hatia, lakini mwaka 2003 alifungwa jela miaka 25 kwa mauaji ya watoto wake watatu, na kuua bila kukusudia mwanawe wa kwanza, Caleb.
Kila mtoto alifariki ghafla kati ya 1989 na 1999, akiwa na umri wa kati ya siku 19 na miezi 19, huku waendesha mashtaka katika kesi yake wakidai kuwa aliwachoma moto.