logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Zimbabwe yawaidhinisha wagombea 11 kuwania urais

Zimbabwe itafanya uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani tarehe 23 Agosti.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri24 June 2023 - 05:03

Muhtasari


•Tume ya uchaguzi ya Zimbabwe ilipandisha ada ya usajili hadi dola 20,000, kutoka dola 1,000 katika chaguzi zilizopita

Baraza la uchaguzi la Zimbabwe limewaidhinisha watu 11 kugombea katika uchaguzi wa urais mwezi Agosti, baada ya wanasiasa wengi kulalamikia ada kubwa ya maombi.

Tume ya uchaguzi ya Zimbabwe ilipandisha ada ya usajili hadi dola 20,000, kutoka dola 1,000 katika chaguzi zilizopita. Ada za nyadhifa za wabunge ziliongezwa kutoka $50 hadi $1,000.

Vyama vya upinzani vilisema ada hiyo ya juu imesababisha athari mbaya kwa demokrasia kwani watu wengi wanapata chini ya dola 300 kwa mwezi.

Zimbabwe itafanya uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani tarehe 23 Agosti.

Tume ya uchaguzi ilifanya kazi hadi usiku wa manane kuwaidhinisha wagombea 11.

Miongoni mwao ni washiriki wawili wakuu, Rais Emmerson Mnangagwa na mpinzani wake mkuu Nelson Chamisa.

Waziri wa zamani wa serikali aliye uhamishoni pia atagombea kama mtu huru.

Idadi ya wagombea ni nusu ya mwaka wa 2018, baada ya watu wengi wanaofahamika kujiondoa wakisema sababu kuwa ada kubwa ya usajili.

Zimbabwe inakabiliwa na uhaba wa fedha, na mzozo wa kiuchumi ambao umepunguza mapato - watu wengi wanapata chini ya dola 300.

Watu takriban 10 walikataliwa, na kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi, hakuna wagombea wanawake walioruhusiwa kugombea.

Wana siku nne za kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa baraza la uchaguzi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved