Trump akana mashtaka ya uchaguzi wa 2020

Rais huyo wa zamani alionekana kwa mara ya tatu ndani ya miezi minne kama mshtakiwa wa uhalifu.

Muhtasari

• Trump aliingia kwenye mlango wa nyuma wa mahakama  Alhamisi alasiri katikati mwa mji mkuu Marekani kutoka eneo la ghasia katika bunge la Marekani ambalo ni msingi wa kesi ya mwendesha mashtaka.

Image: Reuters

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amekana mashtaka ya kula njama ya kutengua uchaguzi wa 2020 katika mahakama ya Washington DC.

Wakati wa kesi ambayo ilichukuwa muda mfupi, alizungumza kwa upole ili kuthibitisha ombi lake la kutokuwa na hatia, jina, umri na kwamba hakuwa chini ya ushawishi wa kilevi.

Baadaye aliwaambia waandishi wa habari kesi hiyo ilikuwa "mateso kwa mpinzani wa kisiasa".

Rais huyo wa zamani alionekana kwa mara ya tatu ndani ya miezi minne kama mshtakiwa wa uhalifu.

Bw Trump aliingia kwenye mlango wa nyuma wa mahakama siku ya Alhamisi alasiri katikati mwa mji mkuu wa taifa hilo, mwendo mfupi kutoka eneo la ghasia katika bunge la Marekani ambalo ni msingi wa kesi ya mwendesha mashtaka.

Takriban washtakiwa 1,000 walioshtakiwa kwa kushiriki katika shambulio dhidi ya Bunge la Marekani mnamo Januari 6, 2021 pia wamefikishwa katika mahakama hiyo.

Hakimu Moxila Upadhyaya alimwambia rais huyo wa zamani asiwasiliane kuhusu kesi hiyo na kumuonya kwamba asipotii agizo hilo hati ya kukamtwa kwake itatolewa, masharti ya kuachiliwa itabatilishwa kwa kupuuza amri ya mahakama.

Waendesha mashtaka waliomba kesi hiyo kusikilizwa kwa haraka.

Bw Trump alizungumza na wanahabari katika uwanja wa ndege wa Reagan akiwa amesimama karibu na msaidizi wake Walt Nauta (kushoto), mshtakiwa mwenzake katika kesi tofauti.
Bw Trump alizungumza na wanahabari katika uwanja wa ndege wa Reagan akiwa amesimama karibu na msaidizi wake Walt Nauta (kushoto), mshtakiwa mwenzake katika kesi tofauti.
Image: Getty Images

Lakini wakili wa Trump John Lauro alisema watahitaji muda zaidi kujiandaa.

Alisema muda wa upande wa mashtaka ulikuwa wa "kushangaza" kutokana na kwamba uchunguzi wenyewe umechukua miaka mitatu.

Madai hayo yaliyowekwa Jumanne katika hati ya mashtaka, ni pamoja na hesabu ya "njama ya kudhoofisha, kuzuia, na kuvuruga shuguli za serikali kwa kutumia ulaghai na udanganyifu".

Bw Trump alishindwa katika uchaguzi wa 2020 na mpinzani wake wa chama cha Democratic, Joe Biden, lakini alikataa kukubali na kuongeza changamoto za wiki kadhaa katika majimbo kadhaa ya Marekani.

Kwa sasa anawania kupeperusha bendera ya Republican katika kinyang'anyiro cha kuongia Ikulu ya White House 2024 na huenda akachuana tena na Biden katika uchaguzi ujao.