Muhtasari
- Maafisa walisema wote waliokuwa ndani ya ndege hiyo - abiria 12 na wafanyakazi wawili - walifariki katika ajali hiyo.
Watu 14 wamefariki katika ajali ya ndege kufuatia hali mbaya ya hewa katika eneo la Amazon nchini Brazil siku ya Jumamosi.
Ndege hiyo ndogo ya propela ilikuwa inakaribia mwisho wa safari yake ya kilomita 400 (maili 248) kati ya Manaus, mji mkuu wa jimbo la Amazonas, na mji wa mbali wa msitu wa Barcelos ilipoanguka.
Maafisa walisema wote waliokuwa ndani ya ndege hiyo - abiria 12 na wafanyakazi wawili - walifariki katika ajali hiyo.
Uchunguzi umeanzishwa kubaini chanzo cha tukio hilo.
Waziri wa usalama wa jimbo la Amazonas Vinicius Almeida alisema taarifa za awali zilidokeza kwamba ndege hiyo ilianguka baada ya kupoteza mwelekeo wakati lipokuwa ikitua Barcelos.