logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Tupatieni ruhusa ya kuingia Gaza ili kuwasaidia watu 11,000 waliojeruhiwa - WHO

Maafisa walisema kumekuwa na mashambulizi 115 kwenye vituo vya huduma za afya

image
na Radio Jambo

Habari17 October 2023 - 13:35

Muhtasari


  • Shirika la Umoja wa Mataifa linakutana na "wafanya maamuzi" leo kufungua njia ya kuelekea Gaza haraka iwezekanavyo - kwa sasa hakuna njia ya kuingia au kutoka.

Shirika la Afya Duniani WHO linasema linahitaji kuingia kwa haraka Gaza ili kutoa misaada na vifaa vya matibabu, huku likionya kuhusu janga la muda mrefu la kibinadamu.

Takriban nusu ya Wapalestina 2,800 waliouawa ni wanawake na watoto huku watu 11,000 wakijeruhiwa katika eneo la Gaza tangu kuanza kwa mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Israel kufuatia mashambulizi mabaya ya Hamas, maafisa kutoka WHO walisema katika taarifa fupi iliyoripotiwa na shirika la habari la Reuters.

Shirika la Umoja wa Mataifa linakutana na "wafanya maamuzi" leo kufungua njia ya kuelekea Gaza haraka iwezekanavyo - kwa sasa hakuna njia ya kuingia au kutoka.

Maafisa walisema kumekuwa na mashambulizi 115 kwenye vituo vya huduma za afya na hospitali nyingi huko Gaza hazifanyi kazi, huku maji na umeme vikiwa vichache.

"Wasiwasi juu ya upungufu wa maji mwilini na magonjwa yanayosababishwa na maji ni mkubwa kutokana na kuporomoka kwa huduma za maji na vyoo," shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Palestina UNRWA lilisema katika taarifa yake. "Watu wataanza kufa bila maji."

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved