logo

NOW ON AIR

Listen in Live

TZ yathibitisha kero la kunguni katika vyuo vikuu baada ya wanafunzi kulalamika mitandaoni

“Hili suala limekuja kwa hali ya kwamba sasa hivi kunguni amekuwa ni mada ya dunia"

image
na Davis Ojiambo

Habari18 October 2023 - 07:45

Muhtasari


  • • Joseph alikiri kwamba waliona na kufuatilia malalamiko ya wanafunzi wa chuo hicho kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kero la kunguni.
Kunguni chuoni UDOM.

Chuo kikuu cha Dodoma, UDOM, nchini Tanzania kimethibitisha kuwepo kwa kero la kunguni wengi katika mabweni ya wanafunzi chuoni humo kufuatia chapisho la mmoja aliyejiita mwanafunzi wa chuo hicho kuanzisha gumzo hilo katika mitanao ya kijamii.

Kwa mujibu wa Rose Joseph ambaye ni mkuu wa kitengo cha mawasiliano katika chuo hicho, suala la kuwepo kwa kunguni si jambo geni kwani kunguni wamekuwepo na si nchini humo tu bali hata katika mataifa ya kigeni yaliyoendelea, akirejelea taarifa za kero la kunguni katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris wiki chache zilizopita.

Joseph alikiri kwamba waliona na kufuatilia malalamiko ya wanafunzi wa chuo hicho kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kero la kunguni ambalo limesababisha baadhi ya wanafunzi kuhama vitandani na kuamua kulala sakafuni.

“Awali ya yote niseme chuo kikuu cha Dodoma kimepokea ama kimeona na kufuatilia katika itandao ya kijamii taarifa zinazozungumzia uwepo wa kunguni kwenye chuo cha UDOM kiasi cha kupeleka baadhi ya wanafunzi kulala chini.”

“Hili kwanza limetufurahisha kwa maana ya kuwa si kutufurahisha kwa namna hiyo bali tumeshangazwa kwa sababu hatukutegemea taarifa za namna hiyo kuandikwa na mwanafunzi anayesema kwamba ni mwanafunzi wa chuo cha Dodoma.”

“Hili suala limekuja kwa hali ya kwamba sasa hivi kunguni amekuwa ni mada ya dunia, Kunguni yuko Ufaransa, sasa kunguni amehamia Dodoma, hakuna shida,” Alisema.

Hata hivyo, Bi Joseph alisisitiza kwamba licha ya kuwepo kwa Kunguni, lakini limegeuzwa kuwa suala la kuchafuana kibiashara akisema kuna baadhi ya watu ambao wanaendesha jumbe za kupotosha kuhusu uwepo wa kunguni kwa lengo la kuchafulia chuo cha UDOM jina.

“Ukweli ni kwamba kunguni ni mdudu ambaye yupo kwenye mashule, kwenye vyuo, na sio UDOM tu. Kwanza itakuwa ni jambo la kushangaza kwamba chuo kikuu hiki chenye wanafunzi Zaidi ya elfu 33 kukosa kunguni,” aliongeza.

Alisema kwamba kwa sasa wanafunzi wapo kwenye likizo nyumbani na walishangazwa sana na suala hilo kuandikwa na mwanafunzi akiwa likizoni nyumbani na si chuoni.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved