Mkuu wa kampuni ya dawa ya kikohozi afungwa jela baada ya vifo vya watoto

Kampuni hiyo, Afi Farma, ilishutumiwa kwa kutengeneza dawa za kikohozi zenye viungo vya sumu.

Muhtasari

•Walihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela na kutozwa faini ya rupiah za Indonesia 1bn ($63,029; £51,7130) kila mmoja.

Image: BBC

Mkuu wa kampuni moja ya Indonesia na maafisa wengine watatu ambayo dawa yao ya kikohozi ilihusishwa na vifo vya watoto zaidi ya 200 wamehukumiwa kifungo cha jela.

Walihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela na kutozwa faini ya rupiah za Indonesia 1bn ($63,029; £51,7130) kila mmoja.

Kampuni hiyo, Afi Farma, ilishutumiwa kwa kutengeneza dawa za kikohozi zenye viungo vya sumu.

Wakili wa kampuni hiyo alisema walikanusha mashtaka ya utepetevu na kampuni hiyo ilikuwa inazingatia kukata rufaa.

Waendesha mashtaka walikuwa wakitafuta kifungo cha miaka saba hadi tisa jela kwa mkuu huyo wa Afi Farma, Prasetya Harahap, na miaka saba kila mmoja kwa washtakiwa wengine.

Mwendesha Mashtaka wa Umma alisema kuwa kati ya Oktoba 2021 na Februari 2022 kampuni hiyo ilipokea vufurushi viwili vya propylene glycol, ambayo hutumiwa kutengeneza dawa ya kikohozi.

Vifurushi hivyo viwili vilikuwa na 96% hadi 99% ya ethylene glycol, mwendesha mashtaka alisema.kemikali zote mbili zinaweza kutumika kama nyongeza kwa vimumunyisho.Wakati, propylene glikoli sio sumu na hutumiwa sana katika dawa, vipodozi na chakula, ethilini glikoli ni sumu na hutumiwa katika rangi na wino wa kalamu.