Kombe la Dunia liko salama baada ya ofisi za raga za Afrika Kusini kuvamiwa na wezi

Picha za CCTV zinaonyesha wavamizi wakigusa Kombe la Dunia kabla ya kuondoka.

Muhtasari

•Waliacha kombe nyuma na badala yake wanaiba Vileo, jezi tano za Springbok zilizosainiwa na kompyuta ndogo nane.

•Msemaji wa Muungano wa Raga wa Afrika Kusini aliambia BBC kwamba mataji yote walioshinda yako salama

Image: BBC

Wezi wameingia katika makao makuu ya Muungano wa Rugby wa Afrika Kusini, ambapo picha za CCTV zinaonyesha wakigusa Kombe la Dunia kabla ya kuondoka.

Wizi huo ulifanyika Jumatatu katika bustani ya ofisi katika vitongoji vya kaskazini mwa Cape Town.

Waliacha kombe nyuma na badala yake wanaiba Vileo, jezi tano za Springbok zilizosainiwa na kompyuta ndogo nane.

Video hiyo inawaonyesha wanaume wakiingia kwenye chumba ambamo nakala ya kombe la William Webb Ellis imehifadhiwa.

Katika picha ambayo imechapishwa kwenye Xna mwandishi wa habari wa Afrika Kusini Yusuf Abramjee, mmoja wa wezi anaonekana akiweka mkono wake wenye glavu kwenye kombe, akiinua kidogo, kabla ya kusonga hadi kabati iliyo chini yake.

Msemaji wa Muungano wa Raga wa Afrika Kusini aliambia BBC kwamba mataji yote walioshinda yako salama

Afrika Kusini ilishinda Kombe la Dunia la Raga mnamo Oktoba 28 baada ya kuishinda New Zealand mjini Paris na kuwa taifa la kwanza kushinda mashindano hayo mara nne.

Nchi ilisherehekea ushindi huo kwa ziara ya siku nne ya ushindi, ambapo timu ilisafiri kwa gwaride kote Afrika Kusini.

Rais Cyril Ramaphosa, pia alitangaza tarehe 15 Disemba kama sikukuu ya umma kusherehekea mafanikio " makubwa ya Springboks".