logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Makumi ya watu wauawa katika mkanyagano wakati wa harakati za kujiunga na jeshi

Takriban watu 37 wamefariki katika mkanyagano kabla ya zoezi la kuwasajili makurutu wa kujiunga na jeshi

image
na Radio Jambo

Habari22 November 2023 - 04:10

Muhtasari


•Takriban watu 37 wamefariki katika mkanyagano kabla ya zoezi la kuwasajili makurutu wa kujiunga na jeshi katika uwanja wa michezo nchini Congo-Brazzaville.

Takriban watu 37 wamefariki katika mkanyagano kabla ya zoezi la kuwasajili makurutu wa kujiunga na jeshi katika uwanja wa michezo nchini Congo-Brazzaville, maafisa wamesema.

Baadhi ya watu walijaribu kupita kwa nguvu katika lango la uwanja wa michezo katika mji mkuu, Brazzaville, na kusababisha mkanyagano huo, wakaazi wamenukuliwa wakisema.

Wiki iliyopita, jeshi lilitangaza mipango ya kuajiri takriban watu 1,500 kati ya umri wa miaka 18 na 25.

Haijabainika ni watu wangapi walijeruhiwa katika ajali hiyo ya usiku kucha.

Taarifa ya serikali ilisema kuwa "kitengo cha kupambana na mgogoro" huo kimeanzishwa, shirika la habari la AFP linaripoti.

Kulingana na shirika la Associated Press, watu wengi kama 700 kwa siku wamekuwa wakijiandikisha katika wiki iliyopita katika vituo vya kuajiri.

Jumatatu usiku, maelfu ya vijana waliripotiwa kujitokeza katika uwanja wa Michel d'Ornano kuwa wa kwanza kwenye mstari Jumanne.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved